Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts
Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts

Thursday, 29 December 2016

SHIGHATINI SEKONDARI

JE, UNA HITAJI ELIMU BORA KWA MWANAO?

 JIBU ni SHIGHATINI SEKONDARI iliyopo Usangi Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro, inawatangazia nafasi za masoo kwa mwaka 2017/2018 kwa wanafunzi wa bweni na kutwa. wote wanaonza form one 2017 na WANAO HAMIA KIDATO CHA PILI, TATU NA NNE

ADA zetu ni nafuu kabisa, kuna mazingira mzauri ya kusomea, na hosteli zipo

mawasiliano
    0784974098 au
    0715974098


  SHIGHATINI SEKONDARI KILICHO BORA ZAIDI..

      "NYOTE MNAKARIBISHWA"

Share:

Friday, 11 November 2016

CEO
KARIBU MVUNGIPLUS  UJIPATIE DONDOO MOTO MOTO NA MAKALA ZINAZOGONGA VICHWA VYA WENGI.

TUNATOA HUDUMA ZIFUATAZO

1. ELIMU YA BIASHARA
2. USHAURI WA MAISHA
3. TUNAUZA NA KUKOPESHA MAWAZO YA BIASHARA
4. UUZAJI ZA VITABU
5. HUDUMA YA USAFIRISHAJI MIZIGO
6. MOTIVATIONAL TALKS.


           TUNAPATIKANA KWA SIMU

0762 198234/ 0719050552/ 0787000146
          BARUA PEPE
mvungifamily@gmail.com

HUDUMIWA KILA MARA


Share:

Sunday, 10 July 2016

AJALI KUBWA YA KUTISHA YATOKEA LEO HUKO MBEYA

Monday, July 11, 2016

Lori lakwepa magari manne, lagonga mengine manne na kuua watu wanne

Licha ya lori lililokosa breki katika Mlima Iwambi nje kidogo ya Jiji la Mbeya, kuyakwepa magari manne, limeyagonga mengine manne na kusababisha vifo vya watu wanne na majeruhi 22. 
Ajali hiyo ilitokea juzi usiku katika mji mdogo wa Mbalizi, Barabara Kuu ya Mbeya - Tunduma, ambako lori hilo liligonga basi aina ya Toyota Coaster na magari madogo matatu.
 Katika tukio hilo, watu watatu walifariki muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitali Teule ya Ifisi na hadi tunakwenda mitamboni walikuwa hawajatambuliwa, huku mwingine aliyetambuliwa kwa jina Philip Cheyo (39) akifariki jana asubuhi katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
 
Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Ifisi, Elimate Sanga alisema walipokea miili ya watu watatu na majeruhi 22 wakiwamo sita waliohamishiwa Hospitali ya Rufaa  ya Mbeya kutokana na hali zao kuwa mbaya. Sanga alisema hadi jana asubuhi, ali- kuwa na wagonjwa 12 waliolazwa. 
Ofisa Muuguzi Msaidizi wa Hospitali ya Rufaa, Lucy Elias alisema Cheyo ambaye alikuwa mmoja wa majeruhi sita, alifariki jana asubuhi akiwa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU). 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari alisema wanachunguza chanzo cha ajali hiyo ingawa taarifa za awali zinaonyesha kuwa lori lilifeli breki wakati likiteremka mlima huo. 
Akisimulia tukio hilo, kondakta wa lori hilo, Wilberd Joseph akiwa wodi ya nne ya Ifisi alisema lilianza kuongeza mwendo wakati wakianza kuteremka mlima huo na ndipo dereva akalalamika halina breki. 
“Nilisikia dereva ananiambia, tuombe Mungu, breki zimegoma kabisa, ndipo lori likazidi kuchanganya na dereva alijitahidi kuyakwepa magari zaidi ya manne hivi, lakini tulipoingia mjini kabisa (Mbalizi), kulikuwa na (basi dogo) Hiace ikitokea upande wa kushoto kuingia barabara kuu, alipolikwepa tela likagonga basi jingine aina ya Coaster lililokuwa limesimama upande wa kulia,” alisema kondakta huyo. 
Alisema baada ya kugonga basi hilo lililokuwa likitokea Tunduma kwenda Mbeya, pia liligonga magari mengine yaliyokuwa nyuma ya Coaster hiyo. 
Mmoja wa majeruhi wa basi hilo, Isack Mwaipaja aliyelazwa katika Hospitali ya Ifisi, alisema walipofika Mbalizi dereva wao hakutaka kuingia stendi na aliamua kuteremsha abiria pembeni mwa barabara kuu ndipo ghafla wakasikia kishindo. 
“Bila kujua kinachoendelea nikajiona nimelowa usoni, kupangusa hivi nikaona damu inavunja usoni, kumbe ni lori lilikuwa limetugonga ubavuni na wale waliokuwa nyuma ya basi ndiyo walioumia sana kwani tela lote liliishia huko,” alisema. 

Share:

Thursday, 30 June 2016

MZIGO WA KODI KUBWA WAANZA LEO RASMIII

Dar es Salaam. Leo ndiyo mwanzo wa utekelezaji wa Sheria Fedha (Finance Act, 2016) iliyopitishwa katika Bajeti ya 2016/17 na Kodi ya Ongezeko la Thamani (Vat) itatozwa kwa huduma za mitandao ya simu, benki na taasisi za fedha.

Akisoma hotuba ya bajeti bungeni hivi karibuni, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango licha ya mambo mengine, alipendekeza kuongeza kodi hiyo katika huduma za benki zinazotozwa ili kupanua wigo wa kodi isipokuwa riba kwenye mikopo.

Vilevile, Waziri Mpango alieleza azma ya Serikali kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia 10 kwenye ada zinazotozwa na watoa huduma katika kutuma na kupokea fedha badala ya ushuru huo kutozwa tu kwenye kutuma fedha pekee.

Akizungumzia uamuzi huo, mtaalamu wa kodi wa kujitegemea, Deogratias Peter alisema ongezeko hilo litawakatisha tamaa wateja wa benki na watumiaji wa miamala ya simu.
Share:
Share:

BREEKING NEWZZ..Wabunge UKAWA Wamaliza Bunge La Bajeti Kwa Mtindo Mpya.....Wavaa Nguo Nyeusi Na Kutoka Nje Wakiwa Na Mabango


Wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani leo asubuhi wameingia bungeni wakiwa wote wamevalia nguo nyeusi walipohudhuria kikao cha 54 cha Bunge la Bajeti mjini Dodoma.

Baada ya Naibu Spika Dk Tulia Ackson kuingia bungeni na kuongoza dua ya kuliombea Bunge, walianza kunyanyua mabango mbalimbali na kutoka nje.
Share:

Thursday, 23 June 2016

Msama amuangukia Mwakyembe kuomba radhi baada gazeti la dira kutoa habari zenye utata


MFANYABIASHARA Alex Msama amemuomba radhi Waziri wa Sheria na Katiba,  Dk. Harrison Mwakyembe kufuatia habari mbili zilizochapishwa katika Gazeti la Dira ya Mtanzania analolimiliki.
 
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msama alisema amejiridhisha kuwa habari hiyo iliyobeba kichwa cha habari ‘Utapeli wa Mwakyembe wamwagwa hadharani’ haikufuata misingi ya uandishi wa habari.

Habari nyingine ambayo imeonekana kumchafua Dk Mwakyembe ni ile ya Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bilioni 2 ambazo zimemuumiza kiongozi huyo.

Alisema yeye kama mmiliki wa gazeti hilo amesikitishwa na habari hiyo na kwamba hatua ya kwanza anayoichukua ni kumuomba radhi Waziri Mwakyembe.

Msama alisema sambamba na kuomba radhi atamfikishia barua Mwakyembe ya kumtaka radhi kwa tukio hilo.

“Nimesikitishwa na habari hii kwa kuwa haikuzingatia misingi ya uandishi wa habari,  ilihukumu na kuonyesha kuwa lengo lake lilikuwa kumharibia jina Waziri Mwakyembe, ninachukua nafasi hii kumuomba radhi nikiwa mmiliki wa gazeti hilo,” alisema Msama.

Aidha Msama alisema hatua nyingine anayochukua ni kumsimamisha kazi mhariri wa gazeti hilo, Mussa Mkama kwa kuwa alishindwa kufanya kazi yake kwa umakini ya kuhakikisha habari anazozipitisha zinafuata misingi ya uandishi wa habari na weledi.

Alisema Mkama alipaswa kuhakikisha anafuata weledi lakini alishindwa kufanya hivyo kwa hiyo anamsimamisha kazi na kwamba hatua nyingine kali za kinidhamu zitafuata.

“Mimi ni mfanyabiashara sijui mambo ya uandishi, nilimuajiri nikiamini atasimamia yale aliyofundishwa chuoni, kwa kuwa ameshindwa inabidi akae pembeni kwanza,” alisisitiza Msama.

Ameahidi kuwa katika Gazeti la Dira ya Mtanzania litakalotoka Juni  27, kwa ukubwa uleule atamuomba radhi Waziri Mwakyembe.

Hivi karibuni  Waziri Mwakyembe aliitisha mkutano wa waandishi wa habari mjini Dodoma akilalamikia kuwa habari mbili za gazeti hilo  iliyochapishwa na Gazeti la Dira ya Mtanzania la Juni 20 na la Juni 23 mwaka huu zililenga kumchafua na kuahidi kuwa atalishtaki kupitia habari hizo mbili.
Share:

Saturday, 11 June 2016

NA HII NDO VITA CHAFU YA CUF NA CCM HUKO PEMBA

SeeBait

Wakati hali ikionekana si shwari visiwani Zanzibar baada ya kuwapo kwa madai ya kutengana, kubaguana na kuharibiana mali, vyama vya CUF na CCM vimetupiana mpira kwa kila kimoja kikimtuhumu mwenzake.

Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria (CUF) Wilaya ya Wete, Mwinyi Juma Ali amesema kuwa chama hicho kinaheshimu misingi ya utawala bora na haki za binadamu na kauli hizo hazina ukweli wowote.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana ofisini kwake, Wete , Mwinyi alisema chama hicho kinasikitishwa na vitendo hivyo hasa vya kufyekwa mashamba na kusababisha hali ya umaskini kwa wananchi .

“Kusema kuwa kitendo cha hujuma hizi kinasababishwa na CUF siyo kweli, kwani chama chetu kinathamini na kuheshimu misingi ya utwala wa sheria na haki za binadamu na hujuma hizi zinatuathiri hata sisi, ” alisema Mwinyi.

Hata hivyo, jana Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omar Khamis Othman alisema hujuma hizo zinapangwa na kuratibiwa na wafuasi wa CUF.

Othman aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi baada ya kutembelea shamba la mihogo na migomba, lenye ukubwa wa eka tano lililofyekwa.

Othman alivitaka vyombo vya ulinzi kuhakikisha wahusika wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwani vitendo hivyo vinaweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Akizungumzia hayo, Mkurugenzi wa CUF, Mwinyi alisema kwamba tangu tuhuma hizo zianze kuelekezwa kwa wanachama wa CUF, hakuna hata mwananchama mmoja ambaye amefikishwa mahakamani wala kutiwa hatiani na kuongeza huo ni msamiati wa propaganda za kisiasa.

Kuhusu migomo inayoendelea, alisema CUF haihusiki na masuala hayo, bali imekuja baada ya viongozi wa Serikali kuwakatisha tamaa wananchi kutokana na chuki zao binafsi

Share:

Friday, 10 June 2016

M PESA, TIGO PESA NA AIRTEL MONEY KODI YAWA BALAAAAA


Wachambuzi na wadau mbalimbali wametoa maoni yao kuhusu Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17, huku watumiaji wa huduma za fedha kwa njia ya simu wakikumbwa na maumivu wa kodi.

Hiyo ni siku moja baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango kuwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 20116/17.

Pamoja na mambo mengine, bajeti hiyo inapendekeza kuongeza ushuru wa vinywaji baridi, maji ya juisi, vinywaji vikali, bia na sigara.

Pia itawagusa watumiaji wa M-pesa, Tigopesa, Airtel Money, Ezypesa   kwa kukatwa Sh 280 kwa kila Sh 1000 watakayotuma.

Jana Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), alisema hatua hiyo ya Serikali kuendelea kutafuta kodi kwa kuzidi kuwaumiza wananchi inakwenda kinyume na matarajio ya Watanzania wengi.

Alisema katika bajeti hiyo ya Serikali na ukusanyaji wa mapato yake, katika kila Sh  1000 itakayokatwa kwa huduma kwenye ATM kuanzia Julai Mosi mwaka huu, Sh 280 zitachukuliwa na TRA.

Zitto alisema hali hiyo pia itawakumba watumiaji wa miamala ya M-pesa, Tigopesa, Airtel Money, Ezypesa ambalo ndilo kundi kubwa la Watanzania wanaotumia huduma hiyo nchini.

Aawali kodi ya bidhaa ilikuwa asilimia 10 lakini kwa hatua ya kuongezwa kwa kodi ya ongezeko la thamani kodi itapaa na kufikia asilimia 28.

Kwa mantiki hiyo, katika kila Sh 100 kodi ni Sh 28 na  katika Sh 1000 kodi ni Sh 280.

Kutokana na hali hiyo kodi ya VAT hulipwa na mtumiaji wa mwisho ambaye anatuma au kupokea fedha, hali ambayo itawaumiza watumiaji wa mwisho.

“Hivyo hivyo katika miamala ya M-pesa, Tigo pesa na kadhalika, katika kila Sh 1000 itakayokatwa kwa huduma kwenye ATM kuanzia Julai 1, 2016, Sh  280 zitachukuliwa na TRA,” alisema Zitto.

Alisema   ameshangazwa na hatua ya Serikali kuongeza kodi ya VAT kwenye utalii hali ambayo inaweza kusababisha Tanzania kupoteza watalii wengi kwa washindani wake kwa sababu itaongeza gharama kwa watalii.

“Kama tunataka kutumia utalii kama kichocheo cha ajira ni vema kufikiria upya suala hili,” alisema.

Akizungumzia mapendekezo ya Serikali katika Sheria ya Kodi ya VAT ili kutoza kodi bidhaa zinazotoka Zanzibar, alisema hatua hiyo inavunja misingi iliyowekwa na sheria ya zamani ambayo ilifanana na ile za Zanzibar.

“Ikumbukwe kuwa Sheria ya Kodi ya VAT ya 2014 ilivunja misingi iliyowekwa ya sheria ya zamani ambayo ilifanana na ile ya Zanzibar. Mapendekezo ya sasa yana madhara makubwa kwa Zanzibar kwa sababu  hakuna atayewekeza Zanzibar ili kufaidika na soko la Bara.

“Biashara nyingi zinazozalisha Zanzibar zitahamia Tanzania Bara. Mapendekezo haya yanaweza kusababisha  mgogoro kati ya pande mbili za Muungano,” alisema.
Share:

Thursday, 9 June 2016

WATOTO SITA WAFA WAKIBATIZWA HUKO ZIMBABWE



Robert Mugabe

Watoto sita wamekufa maji bila kutarajiwa katika sherehe za kubatizwa kwao katika mto nchini Zimbabwe.Watoto watatu walinusurika kufa maji ya mto huo ambao maji yake niya baridi;watoto hao walionekana wakitetemeka kutokana na baridi wakati miili ya wenzao waliokufa maji ikiopolewa majini.

Polisi nchini Zimbabwe wamewatia mbaroni watu wawili ambao ni wafuasi wa dhehebu hilo la Kikristo.

Lakini pia walimjumuisha mama mmoja ambaye alidai kwamba yeye ni nabii ambaye alisema kwamba alifanya jaribio la kufufua wafu wakati wa ibada zake .
Share:

Tuesday, 7 June 2016

MAMLAKA YA HALI YA HEWA (TMA) YATOA MWELEKEO WA HALI YA HEWA KWA KIPINDI CHA JUNI HADI AGOSTI 2016.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa mwelekeo wa hali ya hewa kwa kipindi cha Juni hadi Agosti mwaka huu. Akizungumzia kuhusiana na mwelekeo huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri Bw. Samwel Mbuya alisema “Nchi yetu inatarajia kuwa na hali ya baridi kiasi katika kipindi hiki sambamba na vipindi vifupi vya mvua vinavyotarajiwa kujitokeza katika maeneo machache hususanya ukanda wa Ziwa Viktoria na ukanda wa pwani ya Kaskazini (Visiwa vya Unguja na Pemba).
Katika kipindi cha mwezi Juni hadi Agosti 2016, maeneo mengi ya nchi yanarajiwa kuwa makavu na yenye hali ya baridi kiasi katika majira haya ya kipupwe. Mifumo ya hali ya hewa inaonesha matarajio ya hali ya joto la wastani hadi chini ya wastani katika maeneo yaliyopo Kusini-magharibi mwa nchi. 
Hata hivyo,katika msimu wa Kipupwe wa mwaka huu maeneo mengi ya nchi yanatarajiwa kuwa na joto la wastani hadi juu ya wastani. Aidha, izingatiwe kuwa hali ya ubaridi inatarajiwa zaidi nyakati za usiku hadi mapema asubuhi. “Aliendelea kueleza sababu za hali hiyo kuwa ni pamoja na kupungua kwa joto la bahari katika eneo la ukanda wa Tropiki la bahari ya Pasifiki sambamba na Joto la baharí katikaeneo la magharibi wa bahari ya Hindi kuwa la wastani kwa kipindi cha miezi ya Juni hadi Agosti 2016”. 
Aidha, joto katika bahari ya Atlantiki linatarajiwa kuwa chini ya wastani. Hali hiyo inatarajiwa kusababisha upepo kuvuma kutoka magharibi ukielekea mashariki hususankatika maeneo ya Ukanda wa Ziwa Viktoria. Joto la bahari la juu ya wastani linatarajiwa katika eneo la ncha ya kusini ya bara la Afrika hivyo kuathiri msukumo wa upepo wa kusi.
Kwa upande mwengine, Afisa Uhusiano wa TMA, Bi. Monica Mutoni alitoa msisitizo kwa wananchi kufuatilia taarifa hususan za tahadhari zinazotolewa na Mamlaka kupitia vyombo mbalimbali vya habari, tovuti ya Mamlaka n.k ili kuokoa maisha na mali. Bi. Monica alisema “Hivi karibuni TMA imekuwa ikitoa tahadhari mbalimbali ikiwa ni pamoja na za kuwepo kwa upepo mkali na mawimbi makubwa kwenye ukanda wa Bahari Hindi, Maziwa na nchi kavu hivyo ni vyema wananchi hasa wale watumiaji wa bahari na maziwa kuchukua hatua stahiki pindi taarifa kama hizo zinapotolewa”.
Aidha, TMA ilipongeza sekta mbalimbalipamoja na Taasisi, Mamlaka za Serikali na jamii kwa ujumla kwa hatua stahiki zilizochukuliwa katika kipindi chamsimu wa mvua za Masika 2016 kwa kutumia Taarifa, Agalizona Tahadhari za utabiri zilizotolewa na Mamlaka. Ni wazi kuwa kwa hatua hizo madhara ambayo yangeweza kujitokeza yalidhibitiwa na hivyo kuchangia katika kufanikisha mipango na utekelezaji wa shuguli za kiuchumi na kijamii katika kipindi husika.
Kwa tarifa ya kina kuhusiana na mwelekeo wa hali ya hewa kwa mkoa wako ingia kwenye tovuti ya TMA www.meteo.go.tz au tembelea ofisi zetu

IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
 Meneja wa Kituo Cha Utabiri Kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Bw. Samwel Mbuya akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam kuhusu mwelekeo wa Hali ya joto na mvua katika kipindi cha juni hadi Agosti 2016 ambapo inatarajiwa kuwa na hali ya baridi kiasi na vipindi vifupi vya mvua. Kulia ni Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Bi Monica Mutoni

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)na vyombo vya Habari Leo Jijini Dar es salaam.
Share:

Mzungu afikishwa gerezani kwa kuua mkewe huko Kenya

Mfanya biashara mwenye asili ya uingereza leo hii ametiwa ndani baada ya polis kugundua kwamba alimuua mkewe na kusingizia kwamba amejiua mwenyewe kwa risasi, bw Richard Alden mfanyabiashara maarufu kamuua mkewe bi Grace
Share:

Sunday, 8 May 2016

HUYU NDIYE DONALD TRUMP NA MWEMBWE ZAKE

Bilionea na mgombea uraisi kwa tiketi ya chama cha Republican Tycoon Donald Trump akiwa katika vipindi mbali mbali vya vya matukio yasiyo sahaulika duniani,

Sijui mh huyu ni mtu wa namna gani kwani ni mtaalamu wa kuropoka zaidi ya hata mwimba taarabu wa kipwani.
Share:

Saturday, 16 April 2016

NYETI BANDIA ZA WA DILI DAR

Ni siku chache tu baada ya ulimwengu kugundua zana za kikazi bandia zenye mahadhi ya kureplace uume halisia, wachina bwana acha tu,
   wana dada wa Dar wajitoma rasmi katika ununuaji na utumiaji wa umme bandi almaarufu kama Dildo wakiwa na lengo la kujiridhisha wenye, mwana habari wetu kahoji baadhi ya wana dada wa Dar es salam nakugundua kwamba vifaa hivi vipya vimekuwa bidhaa pendwa kwa wanawake wengi hususani wasichana.
hii ni laana na kufuru ya walimwengu.
Share:

Total Pageviews

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

CEO:KOMBO MVUNGI




HOTLINE:+255719050552 +255762198234


Email:mvungi134family@gmail.com

Dodoma,Tanzania

KARIBU UTANGAZE BIASHARA YAKO BEI NI NAFUU
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Blog Archive

My Blog List

Powered by Blogger.