Showing posts with label MATUKIO. Show all posts
Showing posts with label MATUKIO. Show all posts

Tuesday, 27 September 2016

List Ya Vyuo Vilivyotoa Selection Ya Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Vyuo Vikuu Mbalimbali 2016/2017


Tuesday, September 27, 2016

List Ya Vyuo Vilivyotoa Selection Ya Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Vyuo Vikuu Mbalimbali 2016/2017


Kuona Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Chuo Kikuu 2016/2017,
 
==>Chuo  Kikuu Cha Mwalimu Nyerere   <<bonyeza Hapa>> 

==>Chuo  Kikuu Cha  Udsm,duce Na Muce   <<bonyeza Hapa>> 

==>Chuo  Kikuu Cha  Tumaini Makumira    <<Bonyeza Hapa>>   

==>Chuo  Kikuu Cha Udom  <<bonyeza Hapa>>

 ==>Chuo  Kikuu Cha Ifm <<bonyeza Hapa>>

==>Chuo Kikuu Marian << Bonyeza Hapa>>

 ==>Chuo Kikuu Cbe        << Bonyeza Hapa>>

==>Tumaini-mbeya     << Bonyeza Hapa>> & <<hapa>>

 ==>Chuo Kikuu Mum         << Bonyeza Hapa>>

==>Chuo Mum(Diploma) <<Bonyeza Hapa>>

 ==>Chuo- Stella Maris   << Bonyeza Hapa>>

 ==>Chuo- Kampala-kiu  << Bonyeza Hapa>>

Share:

Tuesday, 6 September 2016

Salum Mwalimu na Wafuasi 18 wa Chadema wapata dhamana

Tuesday, September 6, 2016

Salum Mwalimu na Wafuasi 18 wa Chadema wapata dhamana

Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu imewaachia kwa dhamana Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu na wafuasi wengine 18 wa chama hicho baada ya kukaa mahabusu kwa zaidi ya siku 12.

Kiongozi huyo wa Chadema na wafuasi hao 18 walikuwa wakishikiliwa katika mahabusu za jeshi la polisi kwa tuhuma za kuandaa na kuhamasisha maandamano na mikutano ya Oparesheni ya chama hicho iliyopewa jina la UKUTA, ambayo ilipigwa marufuku na jeshi hilo.

Walifanikiwa kupata dhamana baada ya Hakimu wa Mahakama hiyo kueleza kuwa ameridhia hoja za upande wa utetezi baada ya kusikiliza pande zote mbili na kubaini mapungufu kwenye maombi ya upande wa mashtaka.

Awali, Mwendesha mashtaka aliitaka Mahakama hiyo kuwanyima dhamana washtakiwa hao kwa madai kuwa endapo wataachiwa wataendelea kufanya kosa hilo.

Hata hivyo, Hakimu alitupilia mbali maombi hayo akieleza kuwa wameshindwa kuthibitisha pasipo shaka kuwa endapo washtakiwa hao wataachiwa watafanya tena kosa hilo.

Pia, Hakimu alieleza kukubaliana na hoja ya washtakiwa hao kuwa hati ya kiapo iliyowasilishwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka ilikuwa na mapungufu ya kisheria.

“Ninakubaliana na upande wa utetezi kuwa hati ya kiapo iliyowasilishwa ina mapungufu ya kisheria,” alisema Hakimu baada kupitia na kugundua kuwa aliyesaini hati hiyo sio anayeonekana kuitoa.

Washtakiwa wote walitimiza masharti ya dhamana kwa kuwasilisha wadhamini wawili kila mmoja ambaye ataweka dhamana ya shilingi milioni 3.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alikuwa miongoni mwa watu waliohudhuria mahakamani hapo na kuondoka na Salum na wafuasi hao ambao walifikishwa mahakamani hapo awali chini ya ulinzi mkali. Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 4 mwaka huu

Share:

Friday, 26 August 2016

Mwanamke amkuta mumewe akishiriki ngono na mbwa wake


Mwanamke mmoja amepigwa na butwaa baada ya kumpata mumewe akishiriki ngono na mbwa wao nyumbani Spring Valley, Nairobi

–Inasemekana mwanamke huyo alikuwa amezuru mashambani kupeleka watoto ambapo alirudi nyumbani Nairobi bila kutarajiwa

Mwanamke mmoja alielezea kisa cha kushtua baada ya kumpata mumewe akishiriki ngono na mbwa nyumbani, Spring Valley, Nairobi.

Mwanamke huyo aliondoka nyumbani Jumamosi Agosti 20, kuelekea mashambani Gatanga kupeleka watoto wao.

Walikuwa wamekubaliana na mumewe kuwa angekaa wikendi na wazazi mashambani, hasa baada ya kuacha amemtayarishia chakula mwanamume huyo.

Hata hivyo, alirudi nyumbani ghafla baada ya kukumbuka alikuwa ameacha dawa za mmoja wa watoto wao.

Lakini baada ya kufika nyumbani alipigwa na butwaa baada ya kuingia ndani ya chumba chao cha kulala na kumpata mumewe akishiriki ngono na mbwa wao!

Baada ya kupatikana, mwanamume huyo alivaa nguo haraka na kuondoka nyumbani mara moja, bila kusema chochote
Share:

PICHA CHAFU ZA VUNJA PENZI LA MASOGANGE





Picha chafu z i l i z o v u j a zikimuonesha Video Queen wa Bongo, Agness Gerald ‘Masogange’ akiwa kihasarahasara na mwanaume anayesemekana ni msanii wa Bongo Fleva, Regnald Raymond ‘Reggy’ zimeibua hasira kwa mpenzi wake ambaye ni mwigizaji wa Bongo Muvi, Rammy Galis na kutishia kuvunja penzi lao.


 Chanzo chetu makini kabisa kilisema kuwa ingawaje inadaiwa kuwa picha hizo ni moja ya kurekodi nyimbo inayoitwa Kampa Kampa Tena ya mwanamuziki huyo lakini baadhi ya picha zilizovuja ni chafu na haziko kwenye video ya wimbo huo kitu ambacho kilizidi kuwapa maswali watu mbalimbali ya kuwa kuna kitu kingine zaidi ya picha hizo.



 “Sawa wao wenyewe wanasema kuwa ni vipande vya picha vilivyopo kwenye video ya nyimbo hiyo lakini kwenye nyimbo hiyo ukiitazama vipande hivyo havionekani kabisa,” kilidai chanzo hicho. Mpashaji wetu huyo aliendelea kufunguka kuwa baada ya picha hizo kuvuja mpenzi wa sasa wa Masogange inadaiwa alimpigia simu kijana huyo na kumpa kashikashi huku

akimtaka aache kusambaza picha hizo la sivyo wasije kulaumiana.


Gazeti hili lilipoinyaka habari hiyo lilimtafuta kwanza mwanamuziki huyo ambapo alikana kuwa yeye si mwanzilishi wa kusambaza picha hizo kwa sababu hakuwa na sababu ya kufanya hivyo.



Rammy Galis alipotafutwa kuzungumzia jinsi picha hizo zilivyomchefua hakuweza kupatikana mara moja. Hata hivyo, Masogange alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi alisema: “Unajua kila kukicha watu wanapenda kuibua mambo, ile ni video na mpenzi wangu anaijua, kama kuna kutofautiana na mpenzi wangu picha hizo wala siyo sababu.”
Share:

Saturday, 20 August 2016

Ajali Yaua 1 Maeneo ya Mlimani City Dar




Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitokea ajali mbaya ya gari ndogo ambayo haikuweza kufahamika kwa haraka kutokana na kugongwa na lori lililovuka na kuingia hadi kituo cha mafuta kilichopo jirani na mataa hayo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, gari ndogo ilikuwa ikiendeshwa na mwanamke ambaye mwili wake haukuweza kuokolewa kutokana na kubanwa.
Alipopigiwa simu ili kufafanua kama amepata taarifa za ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa mtu mmoja ndiye aliyefariki na kueleza kuwa yupo kwenye kikao hivyo taarifa kamili ataitoa baadaye.
Share:

BAADA YA KUKATAA KUMPA MKONO RAIS WA ZANZIBAR…CCM wataka Maalim Seif azuiwe kuhudhuria matukio ya kitaifa


seif
Chama cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Serikali kumpiga marufuku Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kuhudhuria hafla na matukio ya kitaifa kutokana na kitendo alichokifanya hivi karibuni kwenye msiba wa Rais wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Aboud Jumbe.
Maalim Seif alikataa kumpa mkono Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein kufuatia msimamo wa chama hicho wa kutoshirikiana na Serikali Visiwani humo, wakipinga kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 na Kufanyika kwa Uchaguzi wa Marudio uliompa ushindi wa kishindo Dkt. Shein baada ya CUF kuususia.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai alisema kuwa ni muda muafaka sasa kwa Serikali kumzuia kushiriki matukio ya kitaifa. Alisema CCM imefadhaishwa na kitendo alichokifanya Maalim Seif na kuwataka watu wote kukilaani.
“Nawaomba watu wasiendekeze sakata hili kwa sababu linamdhalilisha Maalim,” alisema Vuai. “Hatukutarajia kiongozi kama Maalim kufanya kitendo kama kile,” aliongeza.
Hili ni tukio la kwana kwa Maalim kugoma kumsalimia Dkt. Shein. Awali, Dkt. Shein alimtembelea Maalim Seif na kumjulia hali katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam na walizungumza vizuri wakiombeana heri.


Share:

Watakaochakachua Mitihani Kidato cha Nne Kukiona

SeeBait
WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amesema haafiki uchakachuaji kwenye mitihani na kusema wakuu wa shule watakaobainika kufanya udanganyifu huo hawatapona.

Profesa Ndalichako alisema hayo kwenye kikao kati ya Ofisi ya Rais, Tamisemi, Maofisa Elimu wa Mikoa, Wakuu wa shule kongwe na wakuu wa shule zilizoungua moto.

Alisema ikiwa imebaki miezi mitatu kwa wanafunzi wa kidato cha nne kufanya mitihani aliwataka wakuu wa shule kujipanga kupata ufaulu mzuri.

“Bado siafiki suala la uchakachuaji kwenye mitihani wanafunzi waachwe wafanye mitihani wenyewe na si kupitia kamati za ufundi, sasa Wizara inaangalia ubora wa elimu na wakuu wa shule watakaokiuka agizo hilo watachukuliwa hatua,” alisema.

Alisema pia matokeo ya mitihani ya shule za sekondari ya mwaka jana yalimhuzunisha sana lakini anaamini wakuu wa shule watajipanga kuhakikisha wanafunzi wanafanya vizuri zaidi.

“Nilipokuwa Baraza la Mitihani nilisema nisiulizwe kutokana na matokeo kuwa mabaya lakini sasa niko Wizara ya Elimu siwezi kukwepa hilo tena,” alisema.

Waziri Ndalichako alisema watabadilisha mfumo wa namna maofisa elimu watakavyofanya kazi zao ili kuongeza kiwango cha ufaulu katika shule za serikali na kuwataka wakuu wa shule na maofisa elimu kila mmoja ajipange.

Aidha alisema mkuu wa shule ni mdhibiti wa taaluma katika eneo lake na hatakiwi kumuogopa mtu anayemuongoza. Waziri huyo pia alisema katika mtihani wa kidato cha sita uliopita shule 100 za kwanza shule za serikali zilikuwa tatu na kuwa nafasi ya 53 ndio ilishikwa na Ilboru ya Arusha.

“Mpaka namba 100 shule za serikali ni tatu tu, sio kitu cha kawaida hapa ndio mahali pa kuzungumza kama serikali tunashindwa kuonesha mfano tuachie sekta binafsi,” alisema

Share:

INASADIKIWA KWAMBA HUYU NDIYE DAKTARI ALIYETENGENEZA VIRUSI VYA KWANZA VYA UKIMWI HAPA DUNIANI


Pichani ni Dkt Robert Gallo kutoka nchini Marekani aliyetengeneza kirusi cha Ukimwi mwaka 1984,ambacho baadaye kilianza kusambaa dunia nzima na kusababisha vifo vya watu mbalimbali duniani kote 
In April 1984, Dr. Robert Gallo filed a United States patent application for his invention, the HIV/AIDS Virus. Normally, when a patent is filed and approved, as Dr. Gallo’s was, anyone who uses the product or invention owes a royalty payment to the inventor. Thus, holding the intellectual property laws to their fullest interpretations, one must only wonder why Dr. Gallo has yet to file a lawsuit seeking to recover damages from the usage of his invention? As odd as this scenario may sound, it bears need for additional scrutiny. 
The scientific evidence is complete and compelling, the AIDS Virus is a designer bi-product of the U.S. Special Virus program. The Special Virus program was a federal virus development program that persisted in the United States from 1962 until 1978. The U.S. Special Virus was then added as ‘compliment’ to vaccine inoculations in Africa and Manhattan. Shortly thereafter the world was overwhelmed with mass infections of a human retrovirus that differed from any known human disease, it was highly contagious and more importantly, it could kill. 
A review of the Special Virus Flow Chart (“research logic”) reveals the United States was seeking a ‘virus particle’ that would negatively impact the defense mechanisms of the immune system. The program sought to modify the genome of the virus particle in which to splice in an animal “wasting disease” called “Visna”. 
According to the Proceedings of the United States of America, AIDS is an evolutionary, laboratory development of the peculiar Visna Virus, first detected in Icelandic sheep. Recently, American and world scientists confirm with 100% certainty the laboratory genesis of AIDS. This fact is further underscored when one reviews the ‘multiply-spliced’ nature of the HIV ‘tat’ gene and Dr. Gallo’s 1971 Special Virus paper, “Reverse Transcriptase of Type-C virus Particles of Human Origin”. 



Dr. Gallo’s 1971 Special Virus paper is identical to his 1984 announcement of AIDS. Upon further review the record reveals that he filed his patent on AIDS, before he made the announcement with Secretary Heckler. Earlier this year, Dr. Gallo conceded his role as a ‘Project Officer’ for the federal virus development program, the Special Virus. 



The Flow Chart of the program and the 15 progress reports are irrefutable evidence of the United States’ secret plan to cull world populations via the unleashing of a stealth biological microorganism that would ‘waste’ humanity. In light of this true genesis of the world’s most divesting biological scourge, it is the United States that owes ‘royal’ payments to the innocent victims. Each and every victim of AIDS is deserving of a formal apology and a sense of economic closure for an invention of death and despair, perpetrated by the United States. 



The eyes of the world are upon the General Accounting Office’s Health Care Team, under the direction of William J. Scanlon. Between 1964 and 1978, the secret federal virus program spent $550 million dollars of taxpayer money to invent AIDS. It is now necessary to spend whatever it takes to dismantle an invention that has led to the greatest crime against humanity in the history of the world.
Share:
Share:

Friday, 19 August 2016

Mfanyabiashara Moshi Ajimwagia Petroli na Kujipiga Kiberiti


lnawezekana likawa tukio baya lililoacha gumzo na simanzi baada ya mfanyabiashara wa mjini Moshi, Romani Shirima (74), kujiua kwa kujilipua kwa petroli nje ya nyumba yake.

Habari kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zinasema mfanyabiashara huyo alijifunika kwa blanketi, kisha kujimwagia petroli na kutumia kibiriti kuwasha moto ambao ulimlipua na kusababisha kifo chake. 

Ingawa hakuna taarifa rasmi ya nini kiini cha mfanyabiashara huyo kuchukua uamuzi huo mgumu ulioacha maswali mengi, lakini baadhi walidai ni msongo wa mawazo uliotokana na madeni. 
Hili ni tukio la pili kwa mfanyabiashara mkazi wa mkoa wa Kilimanjaro, kwani miaka kadhaa iliyopita, mfanyabiashara anayemiliki hoteli eneo la Marangu alijilipua kwa petroli akiwa katika gari lake. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema  jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi, saa 11.25 asubuhi maeneo ya Mjohotoni. 
Alisema, mfanyabiashara huyo ni mmiliki wa shule ya sekondari ya Merinyo iliyopo mjini Moshi, na kusema kuwa aliamka asubuhi nyumbani kwake na kujimwagia mafuta hayo na kisha kujilipua na kiberiti. 
Kamanda Mutafungwa alisema chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika ingawa kuna maneno yanayoongelewa na watu, lakini hawawezi kuyachukua moja kwa moja na kwamba jeshi hilo linachunguza ili kubaini chanzo chake.
Taarifa za tukio hilo la aina yake zimekuwa gumzo katika maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi na vitongoji vyake, hasa njia aliyoitumia kukatisha uhai wake.
Share:

Friday, 15 July 2016

Kapteni wa jeshi kortini kwa kutishia kumuua polisi



Dar es Salaam. Kapteni  wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), P 12531 Henrick Mahenge (34) mkazi wa Mlimani City, Dar es Salaam amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala leo kujibu mashtaka ya kujaribu kumuua askari wa usalama barabarani.

Kapteni Mahenge ambaye ni mkazi wa Mlimani City,  amepandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan na kusomewa shtaka linalomkabili.

 Akisoma mashtaka, Wakili wa Serikali, Grace Mwanga amedai mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai 12, mwaka huu maeneo ya Mnazi Mmoja wilayani Ilala.

 Mwanga alidai kuwa kuwa mshtakiwa alijaribu kumuua  kujaribu kumuua askari wa usalama barabarani WP  5177  Clesensia Makanyaga.

Mshitakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo.

Hata hivyo, Mwanga alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kwamba hali ya mgonjwa haijulikani hivyo aliomba mahakama izuie dhamana hadi watakapopata uhakika kuhusu hali ya mgonjwa.

Mshtakiwa alipopewa nafasi ya kuelezea kilichotokea, alidai hakutishia kuua na kwamba, yeye ndiye alifanyiwa fujo na kuchaniwa nguo zake.

Alidai alimuona mshitakiwa baada ya tukio na kwamba hakupata taarifa kuwa mlalamikaji yupo hospitali.

Hakimu Hassan alisema kuwa dhamana ipo wazi kwa wadhamini wawili kutoka taasisi zinazotambulika na kuwataka wakaguliwe kwanza kujiridhisha.

 Hata hivyo, alisema mshtakiwa arudi rumande hadi Julai 19, mwaka huu watakapojiridhisha na wadhamini pamoja na kujua hali ya mlalamikaji.
Share:

TANZANIA YA FANYA MAKUBWA KATIKA SEKTA YA AFYA


:)
Share:

Saturday, 9 July 2016

Edward Lowassa ametoa kauli hii kuhusu CHADEMA kufanya maandamano



:)
Share:

Tuesday, 28 June 2016

NJIA RAHISI YA KUPATA MIMBA HARAKA KWA MWANAMKE


1. Kufanya tendo la ndoa mara kwa mara, angalau siku tatu kwa wiki, ikiwezekana on alternate days.
2. Tumia ovulation prediction kit, hiki ni kifaa ambacho kitakusaidia kujua wakati hasa mwanamke ameengua yai na ndio kipindi ambacho mwanamke ana uwezo wa kushika mimba akikutana na mumewe. Ni rahisi kutumia.
3. Fanya tendo la ndoa kabla ya kuengua yai (kabla ya ovulation), huongeza uwezekano wa kushika mimba kuliko kusubiria ovulation au kufanya baada ya ovulation. Kutaneni siku mbili au tatu kabla ya ovulation. Ukitumia ovulation test kit, mkutane kuanzia siku itakapokuwa positive kwani huwa inapredict ovulation kutokea 48 hrs after it tests positive.
4. Usitegemee njia ya kalenda kutabiri uenguaji yai, njia hii kwa kiasi fulani huweza kuwasaidia wale wenye mzunguko wa siku 28, lakini pia haina uhakika wa 100%, wengi wa wanawake hawaengui yai siku ya 14 ya mzunguko wa hedhi, kwa hiyo kutegemea kalenda kutakuchelewesha kupata ujauzito.
5. unapotaka kushika mimba, acha au punguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya pombe, sigara au dawa za kulevya.
6. unapotaka kupata mimba, tendo la ndoa liwe kitu 'enjoyable' na sio tendo 'mechanical' kwa ajili ya kutafuta mtoto. Plan a romantic evening or try something different to spice things up. How you are feeling sexually may increase your chances of getting pregnancy. For women a better orgasm may help pull the sperms into the uterus and for men a better orgasm may increase their sperm count.
7.Kufanya mapenzi katika mtindo (style) ambayo itafanya mbegu za kiume zikae kwa muda mrefu ukeni na hivyo nyingi kupanda kuingia kwenye kizazi na kwenda kurutubisha yai. 'missionary position' ni nzuri zaidi, ambapo mwanaume anakuwa juu, epuka positions
za mwanamke kuwa juu kwani hufanya mbegu zimwagike kwa gravity. Jaribu pia kuweka mto chini ya kiuno ili kukiinua na kufanya mbegu ziingie ndani kwa urahisi zaidi.
Kumbuka kuna asilimia 10 - 25 ya couples ambazo zina matatizo ya infertility lakini vipimo havionyeshi tatizo, inaweza kuwa namna ya kufanya mapenzi ndio ikawa shida, jaribu njia hizo 7 juu.
Share:

GESI YA KUTOSHA YA GUNDULIWA ENEO LA BONDE LA UFA TZ


:)
Share:

ITAMBUE UDOM NA MBWEMBWE ZAKE

    NDUGU MTANZANIA MWENZANGU, MWANA AFRIKA MASHARIKI NA MLIMWENGU
        KWA UJMLA, KWANZA NIANZE KWA KUWASALIMU KWA MUJIBU WA IMANI ZENU  
       IJAPOKUWA MIMI MWANDISHI WAKO SIFUNGAMANI NA ITIKADI YOYOTE.


       SIKU HII YA LEO TAREHE 28 MWEZI WA 6 2016, NAPENDA KUSHARE BAADHI YA
       MAMBO NYETI NANYI ILI MUYAJUE VIZURI KUHUSIANA NA CHUO KIKUU CHA
       DODOMA NA MAMBO YA KIPEE YANAYO PATIKANA NDANI YA CHUO HIKI.

       UDOM! UDOM! UDOM! STAND UP AGAIN

        KWANZA KABISA
     
     1. UDOM NDICHO CHUO PEKEE KIKUBWA AFRIKA MASHARIKI NA CHENYE MIUNDO
         MBINU YA KUTOSHA NA YA KUPENDEZA KULIKO CHUO KINGINE CHOCHOTE KILE
         AFRIKA MASHARIKI.

     2. UDOM NDICHO CHUO PEKEE TANZANIA KINACHOTOA COURSE ZENYE UPEKEE  
         NDANI YAKE KUTOKANA NA KILE KINACHO ITWA UTAALAMU WA UANDAAJI WA
         COURSE

        NB: DEGREE NYINGI ZINAZOTOLEWA NA CHUO KIKUU CHA UDOM NI ZA KIPEE
                 SANA

     JE, UDOM NI CHUO CHA KATA?
 
      NDUGU WALIMWENGU WENZANGU IPO DHANA POTOVU KWA BAADHI YA WATU JUU
      YA CHUO KIKUU CHA DODOMA KWAMBA NI CHUO CHA KATA NA CHUO KINACHO
      CHUKUA WATU WASIO NA UWEZO.
  
      UKWELI WOTE UPO HAPA AISEEE, HEBU JIONEEE MKUU WANGU

      A:  KATIKA VYUO VIKUU VINAVYO TOA WATAALAMU AU WASOMI WENYE MAADILI
           NA WENYE KUKUBALIKA MAENEO YAO YA KAZI NI CHUO KIKUU CHA
           DODOMA  NA HII IMETHIBITIKA KWA RESEARCH ILIYOFANYIKA.

      B:  NI CHUO AMBACHO KINAONGOZA KWA UFUNDISHAJI ULIO TUKUKA.

      C: NI CHUO AMBACHO WANAFUNZI WANAUWEZO WATUAJIRIKA NA HATA KUJIAJIRI
          KUTOKANA NA UWEZO MKUBWA WA KUBADILISHA SEHEMU YA MASOMO YAO
         KUWA UTENDAJI HALISIA (PRACTICABILITY)

       NB:

          a.WANAFUNZI WA UDOM WAMEWEZA KUANZISHA MFUMO WA ONLINE VOTING
         
          b. WAPONJIANI KUANZISHA ONLINE REGISTRATION

          c. WAMEANZISHA ONLINE ASSESSMENT MODEL



      MLIMWENGU MWENZANGU HAPO SASA JIULIZE UDOM NI CHUO CHA NAMNA
      GANI,

   
     EWEEE BABA EWE MAMA MSHTUE MWANAO ASIKUBALI KUPITWA NA KISIMA CHA
     MAARIFA CHANYA YAPATIKANAYO UDOM

   SISI KWETU NI
 
       CENTRE OF EXCELLENCE  NA MWENDOMDUNDO WA ONLY SKY IS LIMIT

   

                UDOM, UDOM UDOM UDOM UDOM UDOM UDOM UDOM


NA
     MVUNGI K.A RAIS WA CHUO CHA ELIMU UDOM
Share:

Monday, 27 June 2016

Charles Kitwanga Aandaa Ibada ya Shukrani

Baada ya kimya cha muda mrefu, hatimaye aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ameibuka na kukabidhi ofisi na akatoa ratiba ya shughuli zake katika Jimbo lake la Misungwi ikiwamo ibada ya shukrani. 
Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa May 20 na Rais John Magufuli baada ya kuingia bungeni na kujibu swali akiwa amelewa, alikabidhi ofisi jana kwa Mwigulu Nchemba ambaye amechukua nafasi yake.
Baada ya uteuzi wake kutenguliwa, Kitwanga alitoweka bungeni na baadaye ilielezwa kuwa alikwenda Israel kabla ya hivi karibuni kurejea nchini na kusema kuwa yote yaliyotokea anamwachia Mungu. 
Hivi karibuni, Rais Magufuli alimhamishia Mwigulu katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi huku Dk Charles Tizeba akimrithi Mwigulu. 
Akizungumza katika mahojiano baada ya kukabidhi ofisi, Kitwanga alisema kila Mtanzania anaweza kufanya kazi iwapo atapewa nafasi huku akinukuu kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ na kwamba amefanya makabidhiano hayo kwa wema na upendo wa hali ya juu. 
Alisema amekabidhi ofisi bila kinyongo kwa sababu Tanzania si nchi yake peke yake bali ni ya wananchi wote. 
Ratiba jimboni 
Akizungumzia ratiba jimboni mwake, Kitwanga alisema Agosti 6, atafanya ibada ya shukrani nyumbani kwake Misungwi kumshukuru Mungu akisema hiyo ni baada ya ziara yake ya wiki sita mfululizo kwa wapigakura wake. 
Ziara hiyo itaanza keshokutwa atakapokutana na kamati ya mipango na fedha kabla ya kufanya kikao na madiwani wote wa jimbo hilo Jumamosi ijayo. 
Alisema Jumatatu ijayo atakabidhi vifaa mbalimbali vikiwamo magodoro na vitanda kwa hospitali ya wilaya na zahanati, vyerahani na kompresa kwa vikundi za ujasiriamali katika hafla itakayofanyika kwenye Stendi ya Mabasi Misungwi: “Hapo nitatoa nafasi ya dakika 10 mpaka 20 kwa waandishi wa habari kuniuliza maswali... lakini nisingependa umbeya... kwangu mimi ni Tanzania kwanza, nawaambia kabisa.” 
Baada ya shughuli hiyo, alisema siku inayofuata atakutana na wenyeviti wa vijiji vyote vya jimbo hilo kupanga namna atakavyofanikisha ziara yake katika maeneo yao, kazi ambayo alisema ataifanya kwa wiki sita mfululizo; “nitafanya ziara siku tano kwa kila wiki mfululizo, zamani nilikuwa nikigawa muda wa kutembelea jimbo na kurudi Dar kufanya kazi sasa nitakuwa huko muda wote. Dar nitakuwa nakuja mara chache tu.” 

Share:

Sunday, 26 June 2016

RAIS MAGUFULI KUTEUA WAKUUWA WILAYA WAPYA


Taarifa kutoka Ikulu ya Tanzania leo June 26 inasema Rais John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko kwenye nafasi za wakuu wa Mikoa pamoja na wakuu wa Wilaya,kwenye mabadiiko hayo amewateua jumla ya wakuu wa wilaya 139.
Mabadiliko haya yanamhusu aliyekua mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi.Zainab R. Telack kuwa mkuu mkoa wa Shinyanga  ambaye anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekua mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi.Anna Kilango Malecela.
Mwingine aliyehusishwa na mabadiliko haya ni pamoja na Dkt Binilith Satano Mahenge kuwa mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Dkt. Satano anajaza nafasi ilyoachwa wazi na aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam ambapo atapangiwa majukumu mengine.
Mwingine  aliyeteuliwa ni Dkt. Charles F Mlingwa ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Mara  na anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw.Stanslaus Magesa Mulongo  ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Nimeipata pia List ya wakuu wa Wilaya wapya mtu wangu nimekuwekea na List ya wilaya zao.
1
2
3
4
5
6
7


:)
Share:

Total Pageviews

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

CEO:KOMBO MVUNGI




HOTLINE:+255719050552 +255762198234


Email:mvungi134family@gmail.com

Dodoma,Tanzania

KARIBU UTANGAZE BIASHARA YAKO BEI NI NAFUU
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Blog Archive

My Blog List

Powered by Blogger.