Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

Friday, 11 November 2016



  WANAJANGWANI WATOA RAMBIRAMBI ZA KIFO CHA MBUNGE  ALI TAHIR

Uongozi wa klabu ya soka ya Yanga unasikitika kutangaza kifo cha mwanachama wake Mhe Hafidh Ally Tahir kilichotokea mjini Dodoma tarehe 10/11/2016.

Mhe Hafidh Ally Tahir – ambae Pia alikuwa mbunge wa CCM Jimbo la Segerea Dimani Zanzibar amefariki akiwa anapitiwa matibabu katika hospital ya General mkoani Dodoma.
Mheshimiwa Hafidh Ally Tahir alikuwa ni miongoni mwa Marefa wa mwanzo wa FIFA barani Afrika ambapo amechezesha mechi za soka za kimataifa.

Katika maisha yake, Mheshimiwa Hafidh Ally pia alikuwa mtangazaji wa iliyokuwa Redio Tanzania ambapo miongoni mwa manguli aliyofanya nayo kazi ni Marehemu David Wakati “Magunia”.

Katika utawala wa Rais wa Tano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ); Mheshimiwa Hafidh Ally alikuwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Aidha Mheshimiwa Hafidh Ally ashawahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Rahaleo.

Mheshimiwa Hafidh Ally alikuwa ni mwanasoka hadi dakika ya mwisho kwani alichezea timu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Yanga iliyoinyuka ile timu shindani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Simba, ambapo alifunga magoli matatu katika mechi hiyo.

Siku moja kabla ya mauti kumfika Mheshimiwa Hafidh Ally alichaguliwa kuwa Katibu wa Timu hiyo ya Bunge, chini ya Uenyekiti wa Mbunge wa Kilolo Mheshimiwa Mwamoto.

Mchango wake Mkubwa utakumbukwa daima na sote tunaungana na familia yake, wananchi wa jimbo la Dimani chini ya Mwakilishi Mheshimiwa MwinyiHaji Makame Mwadini, Wazanzibari wote chini ya Kiongozi wetu Dkt Ali Mohamed Shein – Rais Wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na pia Watanzania wote chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt John Pombe Joseph Magufuli.

Yanga inatuma salamu za rambirambi maalum kwa Waheshimiwa Wabunge wote na Watumishi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Uongozi Mahiri wa Mheshimiwa Job Ndugai (Mb) – Spika wa Bunge.
Uongozi was Yanga utashiriki kikamilifu katika mazishi huko visiwani Zanzibar.

Imetolewa na Uongozi,
Young Africans Sports Club
Share:

Sunday, 10 July 2016

ALICHO SEMA MA WA RONALD BAADA YA MWANAE KULIA UWANJANI

:)
Share:

Monday, 27 June 2016

MASTAA 6 WA WAFATA NYAYO ZA MESSI KUTUNDIKA DARUGA ARGENTINA

Messi-Mascherano
Hii ni siku mbaya kwa soka la Argentina, baada ya kushindwa kutwaa taji la Copa America kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Chile, wachezaji wa Argentina mmoja baada ya mwingine wamekuwa wakitangaza kustaafu kuichezea timu yao ya taifa.
Mchezaji wa kwanza kutangaza kustaafu kuitumikia timu hiyo alikuwa Leo Messi ambaye alitangaza uamuzi huo muda mfupi baada ya mchezo dhidi ya Chile kumalizika.
Muda mfupi baadaye striker wa Manchester City Sergio Aguero na mlinzi wa kati wa FC Barcelona Javier Mascherano nao pia walitanga kuachana na timu soka la kimataifa.
Kama vile haitoshi, ripoti kutoka Amerika ya Kusini zinadai kuwa, Angel Di Maria, Ezequiel Lavezzi, Gonzalo Higuain na Lucas Biglia nao pia wameamua kutundika daruga kuitumikia Argentina.
Laikini kocha wa timu hiyo Tata Martino hajajukua uamuazi wa kuikacha timu hiyo.


Share:

Thursday, 23 June 2016

RATIBA YA EURO


Baada ya mechi za makundi kumalizika jana, sasa inafuata hatua ya 16 bora ya michuano ya Euro 2016. Ni baada ya mechi kali na za kusisimua zilizoshuhudia Ureno na Ireland zikipenya dakika za mwisho .

Kuna mechi kadhaa ambazo zinaturudisha kwenye historia ya mashindano haya na zinatarajia kuwa na presha kubwa kuanzia kwa wachezaji, mabenchi ya ufundi na hata mashabiki pia.

Italy v Spain inatarajiwa kuwa mechi kali mchezo ambao unazirejesha timu hizo kwenye kumbukumbu ya mchezo wa fainali ya Euro 2012 ambao Spain walishinda kwa bao 4-0.

Spain pia iliifunga Italy kwenye michuano ya Euro 2008, kwa hiyo Italy vichwani mwao watakuwa na kibarua cha kulipa kisasi watakapokutana siku ya Jumatatu.

Ufaransa v Ireland ni game nyingine ianayotazamwa kwa uzito wa aina yake licha ya Ireland kuonekana kama vibonde mbele ya Ufaransa. Goli la mkono la Thierry Henry bado linawakumbusha machungu Ireland pale waliposhindwa kufuzu kucheza michuano ya kombe la dunia.

Ratiba kamili ipo kama ifuatavyo:

Switzerland v Poland (Jumamosi)

Wales v Northern Ireland (Jumamosi)

Croatia v Portugal (Jumamosi)

France v Republic of Ireland (Jumapili)

Germany v Slovakia (Jumapili)

Hungary v Belgium (Jumapili)

Italy v Spain (Jumatatu)

England v Iceland (Jumatatu)
Share:

Monday, 20 June 2016

MO BEJALA YA MFUNDISHA YANGA KITU MURUWAAA

Usiku wa Jumapili June 19, Yanga ilipoteza mchezo wake wa kwanza wa michuano ya shirikisho Afrika mbele ya MO Bejaia ya Algeria na kudosha pointi tatu .

Yassin Sahli ndiye aliyewapa machungu wanajangwani dakika ya 20 tu pale alipoifungia timu yake bao bekee kwenye mchezo huo lililodumu kwa dakika zote za mchezo huo.

Inawezekana haukuliona goli hili, angalia video ya bao hilo hapa chini…MO Bejaia 1-o Young Africans



Share:

Sunday, 19 June 2016

MDOGO WAKE MWAPE ASAINI RASMI KWA WANAJANGWANI

Obrey akisaini mkataba
Mzambia Obrey Chirwa maarufu kama cholo hatimae ametua rasmi juzi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere na kupokelewa na baadhi ya mashabiki wa Yanga ambao walijitokeza katika uwanja huo. Baada ya kuwasili Obrey alienda moja kwa moja katika makao makuu ya wanajangwani hao mitaa ya twiga na jangwani.

Baada ya kufika alifanikiwa kusaini rasmi kandarasi ya miaka miwili ya kuwatumikia wanajangwani hao maarufu kama wakimataifa. Obrey anakuwa ni Mzambia wa pili kujiunga na wanajangwani hao baada ya Mzambia mwenzake Davies Musonda Mwape aliyeichezea Yanga mpaka 2012 na hatimae kuondoka.
Obrey anaeichezea timu ya taifa ya Zambia chini ya miaka 23 ni mmoja wa washambuliaji wa pembeni hatari wenye chenga za maudhi na anaejua kuzifumania nyavu vilivyo.

amesajiliwa kutokea fc Platinum ya Zimbambwe kwa zaidi ya dola laki moja za kimarekani ambazo ni zaidi ya shilingi milioni mia mbili za kitanzania. Obrey anakuja kuchukua nafasi ya Mniger Isofou Aboubaca ambaye amesitisha mkataba na wanajangwani hao baada ya kutoridhishwa na kiwango chake.

Cholo anakuja kuungana na Donald Ngoma na Thabani Kamusoko ambao walicheza pamoja fc Platinum, kombinesheni ya Ngoma Tambwe na Obrey inategemewa kuja kuisaidia Yanga katika mashindano yanayoendelea hivi sasa ya kombo la shirikisho amabayo leo Yanga wanacheza na FC Mo Bejaia ya Algeria majira ya saa 6;45 usiku.
Share:

Saturday, 11 June 2016

MANJI ATUSUA UCHAGUZI NDANI YA YANGA


Dar es Salaam. Matokeo ya awali yanaonyesha kuwa Mwenyekiti wa Yanga anayetetea nafasi yake, Yusuph Manji anaongoza kwa kura 1,468, na hakuna zilizomkataa, huku mbili zikiharibika.

 Akizungumzia uchaguzi huo ambao kura zimeendelea kuhesabiwa hadi asubuhi ya leo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha klabu hiyo, Jerry Muro amesema Clemence Sanga anaongoza katika nafasi ya Makamu mwenyekiti kwa kujikusanyia kura 1,428 dhidi ya mpinzani wake, Tito Osoro aliyekuwa amepata kura 80.

 Hadi taarifa hizi zinapatikana kutoka Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam, klabu hiyo ilikuwa inaendelea na mchakato wa kuhesabu kura za wajumbe.Hata hivyo, Muro amesema matokeo kamili yatatolewa leo.
Share:

matokeo ya kwanza uchaguzi wa yanga kwa nafasi ya mwenyekiti na makamu wake


Najua mashabiki na wanachama wa Yanga wote walikuwa wanasubiri kwa hamu kujua matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu wa Yanga katika nafasi mbalimbali, hususani ya mwenyekiti na makamu wake.
Katika nafasi ya mwenyekiti Yusuph Manji ndio alikuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo, kura za awali zimetangazwa yeye amepata jumla ya kura za ndio 1468, hapana 0 na kura mbili ndio zimeharibika.
Kwa upande wa nafasi ya makamu mwenyekiti Clement Sanga amepata jumla ya kura 1428 wakati mpinzania wake Ossoro amepata jumla ya kura 80, matokeo rasmi ya uchaguzi mkuu wa Yanga yatatangazwa kesho Jumapili ya June 12 2016.
NA MVUNGI K.A
Share:

Friday, 10 June 2016

HILI NDO JINA LA GOZI JIPYA KWENYE URO 2016

 Kindakindaki cha ligi ya Euro 2016 inaanza  leo nchini Ufaransa ambapo kutakuwa na mchezo mmoja unaohusisha wenyeji Ufaransa watakapambana vikali na Romania katika mchezo utakaopigwa kunako dimba la Stade de France majira ya saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Kama ilivyoada katika michuano ya Ulaya, Amerika na hata dunia kwa ujumla huwa kunakuwa na mpira maalum uliondaliwa kwa ajili ya michunao husika.

Katika michuano ya Euro mwaka huu, mpira utakaotumika unajulikana kwa jina la Adidas Beau Jeu. Beau Jeu ni jina la kifaransa lenye maana ya ‘Beautiful Game’ au ‘Beautiful Play’ ambapo kwa Kiswahili maana yake ni Mchezo mzuri.

Huu ulizinduliwa na Adidas na kutambulishwa na mchezaji wa zamani wa Ufaransa Zinedine Zidane mwezi Novemba mwaka jana.

Mpira huu unajumuisha baadhi ya vitu kama Adidas Brazuca.  Una rangi ya bluu, nyeusi na machungwa huku ukiwa umeandikwa ‘EURO 2016’.
Share:

Thursday, 9 June 2016

YANGA MAMBO BUM BUM KWA TAMBWE NA NGOMA SOMA ZAIDI KUJIONEA

Mabingwa na wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika, timu ya Yanga SC tayari imeanza kambi ya maandalizi jijini Dar es Salaam kujiwinda na mchezo wao wa kwanza hatua ya makundi dhidi ya MO Bejaia ya Algeria.

Yanga imefuzu kwa nane bora ya michuano ya CAF kwa mara ya nne huku ikiwa ni mara yao ya kwanza kufika hatua hiyo katika Confederation Cup. Chini ya wakufunzi, Hans Van der Pluijm, Juma Mwambusi na Juma Pondamali.

Kikosi hicho kilichotwaa kwa mara ya pili mfululizo ubingwa wa ligi kuu mwezi Mei kimeingia kambini kikiwa na wachezaji wake wapya, Hassan Kessy, Juma Mahadhi na Vicent Andrew ambao wamejiunga na timu hiyo wakitokea klabu za Simba SC, Coastal Union na Mtibwa Sugar.

Yanga itaanza kucheza ugenini Juni 17 imepanga kuweka kambi ya wiki moja nchini Uturuki kabla ya kutua nchini Algeria kusaka ushindi wa kwanza wa kihistoria katika ‘ardhi ya Mwarabu.’

“Tayari tumeanza kambi ya maandalizi kuelekea michuano ya CAF wiki hii na wachezaji wote tayari wameshawasili na kuanza mazoezi.” anasema mkuu wa kitengo cha habari wa klabu hiyo Jerry Murro.

“Amis Tambwe na Donald Ngoma hawakuonekana katika mazoezi ya kwanza lakini tayari wameshawasili. Kutokana na sababu za kimazingira, kule walipotoka hadi kufika Dar es Salaam tumeona wapumzike kwanza lakini wataanza mazoezi wiki hii.”

“Tunategemea kuweka kambi ya wiki moja nchini Uturuki au tunaweza kuondoka kutoka hapa hadi Algeria kwa ajili ya mchezo. Itategemea ratiba ya ndege na urahisi wa kufika Algeria. Bado tupo katika mazungumzo na mashirika ya ndege na tutawaambia kitakachojiri kwa maana ni lazima tufanye hivyo.”

Kwa ukaribu zaidi, tafadhali unaweza ku-LIKE PAGE yangu BSports. Utapata Updates za michuano mbalimbali.
 
Share:

IBRAHIMU TWAHA ASAINI MTIBWA SUGAR FC



Share:

DAN ALVES AONDOKA RASMI BARCA NA KUACHA HAYA YA FUATAYO

Dani Alves ni moja ya wachezaji waliocheza Bracelona kwa mafanikio makubwa sana. Ameitumikia kwa uaminifu klabu hiyo kwa takriban misimu nane. Alves anaondoka rasmi Barcelona na kuelekea Juventus ya nchini Italy. Baada ya msimu huu kumalizika, aliandika ujumbe mzito sana kuwashukuru mashabiki, wachezaji pamoja na viogozi wa Barcelona. Katika kipindi chote alichodumu klabuni hapo amefanya mambo makubwa sana, lakini haya ni baadhi kati ya hayo yote.

Alves alijiunga na Barcelona katika usajili wa majira ya joto mwaka 2008 baada ya kuitumikia Sevilla kwa miaka sita kipindi hicho akiwa na miaka 25. Wakati akijiunga na Barcelona aliyekuwa rais wa Barcelona Joan Laporta alimtunuku kama ‘beki bora wa kulia duniani’ akithibitisha ubora wake kutokana na ada ya Euro milioni 35 aliyonunuliwa. Ada hiyo ya uhamisho ilimfanya Alves kuwa  mchezaji wa pili kununuliwa kwa kitita kikubwa zaidi katika historia ya timu hiyo  kwa wakati huo.

Katika mchezo wake wa kwanza alianza na kikosi chenye wachezaji hawa: Golini alikuwa Victor Valdez, kulia Alves mwenyewe, kushoto Erick Abidal, nne na tano kulikuwa na Carlos Puyol na Marquez, nafasi ya kiungo kuliwa na Xavi Hernandez, Yaya Toure na Andres Iniesta, safu ya ushambuliaji iliundwa na Lionel Messi, Thierry Henry na Samuel Eto’o.

Goli lake la kwanza alifunga kwenye mchezo dhidi ya Almeria Oktoba. Katika mchezo huo, Samuel Eto’o alipiga hat-trick huku goli lingine likifungwa na Thierry Henry.

Alves alishiriki kikamilifu kuweka historia msimu wa 2008/09, akiwa moja ya wachezaji waliofanikisha kuipa Barcelona makombe matatu kwa mpigo kwa msimu (treble). Akiwa chini ya Pep Guardiola, Alves alicheza michezo ya ligi 34, 12 ya UEFA Champions League na nane ya Copa del Rey.

Akiwa na Barca kwa msimu wake wa pili, Alves alifanikiwa kufikisha michezo 100 ambapo ilikuwa ni Mei 4, 2010. Katika mchezo huo dhidi ya Tenerife Barca walishinda magoli 4-1, ambapo Alves alitoa pasi mbili za mabao (assists), moja kwa Bojan na nyingine kwa Lionel Messi.

Januari 25 katika dimba la Cam Nou, kwa mara ya kwanza Alves alifanikiwa kuwafunga Real Madrid baada ya kuachia shuti kali kutoka nje ya penati boksi na kutinga wavuni. Hiyo ilikuwa ni katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Kombe la Mfalme (Copa del Rey) ambapo Barca walifanikiwa kusonga mbele.

April 3, 2012, katika mchezo wa nusu fainali ya UEFA Champions League dhidi ya AC Milan, Alves alifanikiwa kutimiza michezo 200 akiwa na Barca huku akiweka kibindoni magoli 15 mpaka siku hiyo. Katika mchezo huo Barca walishinda mabo 3-1, mchezo uliochezwa katika dimba la Camp Nou.

Katika msimu wa 2013/14, Alves aliamua kubadilisha namba ya jezi yake na kuvaa namba 22 akii-dedicate kwa Erick Abidal ambaye alikuwa akiondoka kutokana na matatizo ya afya yaliyokuwa yakimsumbua. Abidal alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya ini.

Msimu huo huo wa 2013/14, Alves alikuwa nyota wa mchezo wa 16 bora kati ya Barcelona na Manchester City. Akifunga katika mechi zote mbili. Mchezo wa kwanza walishinda magoli 2-1, wa pili walishinda magoli 2-1.

April 20 mwaka 2014, katika mchezo dhidi ya Athletic Club Bilbao kwenye dimba la Camp Nou, Alves alimzidi Phillip Cocu na kuwa wa pili katika orodha ya wachezaji wa kigeni waliocheza mechi nyingi zaidi katika historia Barcelona kwa kucheza michezo 293. Kuondoka maana yake ni kwamba Lionel Messi ataendelea kushikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kwa kucheza mechi 531.

Alves ameondoka Barca akiwa amecheza michezo 391.

Msimu wa 2014/15, Alves alisherehekea kutimiza michezo 300 akiwa na Barcelona katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya APOEL.

Msimu wa 2015/16, Alves alirudia tukio la kubadilisha namba ya jezi kwa mara nyingine tena baada ya kuamua kuachana na jezi namba 22 iliyokuwa ya Abidal na kuvaa jezi namba sita maalum kwa ajili ya kumuenzi  Xavi ambaye ni Legend wa klabu hiyo aliyekuwa akiondoka.

Kuondoka kwa Alves inawezekana ni habari mbaya sana kwa Barcelona, lakini mbaya zaidi kwa Messi ambaye ndiyo amepata pasi nyingi za magoli (assist) kutoka kwa Dani Alves kwa kipindi chote cha miaka nane aliyohudumu klabuni hapo.

Goli lake la mwisho alifunga katika msimu wa 2015-16, katika mchezo wa Copa del Rey dhidi ya Villanovense. Msimu huo pia alichangia kwa kiasi kikubwa Barcelona kuchukua treble.

Katika kipindi kisichopungua wiki mbili kabla ya kutangaza kuondoka kwake, Alves alicheza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Sevilla kwenye kombe la Copa del Rey, ambapo Barca walishinda na kuchukua kombe hilo. Ikumbukwe mchezo huo ulikuwa na maana kubwa sana kwake kutokana na kucheza na Sevilla, timu ambayo ilimtambulisha katika ulimwengu wa soka la Ulaya.

Sasa ni rasmi anaondoka Barcelona akiwa ameacha historia kubwa. Kwa muda wake wote klabuni hapo, ameshinda kila kombe ngazi ya klabu. La Liga mara sita. Champions League matatu, Copa del Rey matatu, European Super Cup matatu, Spanish Super Cup manne na matatu ya Club World Cup.
Share:

CR7 AMZIDI MAYWETHER KWA KULIPWA DAU KUBWA DUNIANI

Cristiano Ronaldo has become the top earning athlete in the world after making £61million last year alone beating long-term leader Floyd Mayweather Jnr into first place. The retired boxer, who fought just once within the last 12 months, earned £30million.
Ronaldo struck a £38.5million-a-year salary with Spanish giants Real Madrid. Plus his endorsement deals with Nike, watchmaker Tag Heuer and nutrition supplements group Herbalife were worth £22million.
His football rival Lionel Messi is second on the list raking in £56million within the last year.

Share:

Wednesday, 8 June 2016

MESSI NA CR7 WAINGIA NDANI YA KUMI BORA YA MATAJIRI DUNIANI

Forbes wametoa list ya wanamichezo 100 matajiri duniani, kwa upande wa TOP 10 mchezo wa soka ambao ndio unatazamiwa kuwa unaingiza hela nyingi, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi pekee ndio wamefanikiwa kuwa na utajiri uliowafaya waingie TOP 10.
top 10
Top 10 ya wanamichezo matajiri duniani
Ronaldo ndio ameongoza katika list ya wanamichezo matajiri duniani kwa kuwa na utajiri wa dola milioni 88 ambazo ni zaidi ya bilioni 190 za kitanzania, Lionel Messi ameshika nafasi ya pili kwa kuwa na utajiri wa dola milioni 81.4 ambazo ni zaidi ya bilioni 178 za kitanzania.
Cristiano Ronaldo utajiri wake wa dola milioni 32 ambazo ni zaidi ya bilioni 70 za kitanzania unatokana na mikataba ya matangaza kupitia account zake za social network kama twitter, instagram na facebook.
Share:

SHARAPOVA AFUNGIWA KUCHEZA TENNIS MIAKA 2

Maria Sarapova ni miongoni mwa wanawak matajiri duniani, ambaye ni mcheza tennis maarufu. Maria Sharapova ameitikisa wimbi la michezo duniani baada ya kufungiwa kucheza Tennis kwa muda wa miaka miwili, na hii ni mara tu baada ya kunaswa na vipimo vya kisasa juu ya kile kinacho itwa utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu.
sharapooShirikisho la Tennis la kimataifa duniani (ITF) limemfungia Maria Sharapova baada ya kugundua kuwa amekuwa akitumia dawa hizo za kusisimua misuli aina ya Meldonium kwa muda mrefu.
Shirikisho hilo limetangaza rasmi June 8 2016 kuwa mrembo huyo hatoruhusiwa kucheza tennis kwani amekiuka sheria za michezo, ingawa imetangazwa rasmi kufungiwa kwake, Maria Sharapova anasema yeye amekuwa akitumia  dawa hizo kwa  matibabu ya moyo tangu mwaka 2006.
Share:

BRAZILI YA MCHAPA HAITI GOAL 7-1


Timu ya taifa ya Brazil  leo alfajiri ya June 9 2016 ilishuka dimbani kucheza mchezo wake wa pili wa michuano ya Copa America dhid ya timu ya taifa ya Haiti, katika mchezo huo Brazil ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 7-1.
Brazil ambao walikuwa na wachezaji wao nyota kasoro Neymar Junior, walianza kupata goli la kwanza kupitia kwa Philipo Coutinho aliyefunga magoli matatu yaani hat-trick kuanzia dakika ya 14, 29 na 90, Renato Agusto aliyefunga magoli mawili dakika ya 35 na 86, Gabriel dakika ya 59 na Lucas Lima dakika ya 57, wakati goli pekee la Haiti lilifungwa na James Marcelin dakika ya 70.
Kwa matokeo hayo Brazil wanakuwa wanaongoza katika msimamo wa Kundi B kwa jumla ya point 4 wakifuatiwa na Peru wenye point moja, hiyo inatokana na wao kutoa sare mchezo wa kwanza dhidi ya Ecuador, ushindi wa 7-1 kwa Brazil unajaribu kufuta machozi kwa upande wao, kwani walishawahi kufungwa goli 7-1 na timu ya taifa ya Ujerumani tena katika ardhi yao ya Brazil wakati wa michuano ya Kombe la dunia.
Share:

Tuesday, 7 June 2016

ARGENTINA YA MCHAPA CHILE GOLI 2-1 COPA AMERICA

leo Alfajiri katia mechi ya kukata nashoka baina ya Argentina na Chile kwenye michuano ya COPA AMERICA inayorindima kunako bara la Marekani.
 
Argentina walijipatia bao la kwanza dakika ya 50 kupitia kwa mshambuliaji wa pembeni anayekipiga kunako klabu ya PSG, Angel Di Maria, dakika 9 baadaye Chile walifanya chambulio la nguvu langoni mwa Argentina lakini halikuzaa goli na papo hapo Argentina wakatumia mwanya huo kufanya 'Counter Attack' langoni mwa Chile na bila ajizi Ever Banega akatumbukiza bao la pili, na kufanya ubao wa matokeo kusomeka 2-0. Katika dakika za majeruhi Jose Fuenzalida akaipatia Chile bao la kufutia machozi. Mwisho wa mchezo Argentuna 2, Chile 1.

Kwenye kipute cha awali kwa siku hii kilichopigwa ndani ya dimba la Levs jijini Califonia, Panama iliifunga Bolivia kwa mabao 2-1,washindi walianza kujipati bao kupitia kwa mchezaji Alberto Quintero's kunako dakika ya 10 tu ya mchezo alipounganisha kwa mtindo wa "slide motion" krosi ya Blas Perez,bao lililodumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili Bolivi walijipapatua na kusawazisha bao kupitia kwa Juan Carlos Arce baada ya mabeki wa Panama kuzubaa kuuondoa mpira langoni mwao.Kunako dakika ya 87 Panama walihanikiza ushindi kwa kupachika bao la pili lililofungwa na mshambulizi Blas Perez.
Leo ni
MAREKANI vs COSTA RICA
COLOMBIA vs PARAGUAY
Share:

Friday, 27 May 2016

MAN U WALAMBA DUME

Waungwana wapenzi wa blog yetu leo hii tarehe 27/5/2016 siku ya Ijumaa club ya Man United imetangaza na kumpokea rasmi kocha machachari na  mtaalamu Jose Mourinho, kuwa kocha wa Man U  kwa ofa tamu ya mkataba wa miaka mitatu na kufanya kocha huyo raia wa Ureno kuhudumu na magwiji wa soka Uingereza kwa muda wa miaka mitatu.
Share:

Saturday, 7 May 2016

MCHEZAJI WA SOKA APOTEZA UHAI WAKE NDANI YA DIMBA dakika ya 67

Hii ndio video ya mchezai aliyepoteza uhai wake akiwa uwanjani baada ya matatizo ya moyo kumshika gafla na kuanguka uwanjani, Patrick Ekeng alifariki dunia akiwa anakipiga  Romani, ilikuwa ni mechi yake dhidi ya Viitorul, ambapo aliingia uwanjani dakika ya 62 kipindi cha pili, na mnamo dakika saba mbele alianguka gafla na kukimbizwa hospitalini ambapo ndipo alipoupoteza uhai wake.
alikuwa mchezaji kinda mwenye umri wa miaka 26.
Share:

Saturday, 16 April 2016

YANGA YA ZIDISHA WIMBI LAKE LA USHINDI DHIDI YA MTIMBWA

   DAR-ES SALAAM YANGA AFRICAN IMEIBUKA KIDEDEA DHIDI YA MTIBWA SUKARI, KATIKA MCHEZO AMBAO ULIKUWA NA VUTA NI KUVUTE,


    TWENDE SAWA NA VIDEO HIII YA MCHEZO WENYEWE.
Share:

Total Pageviews

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

CEO:KOMBO MVUNGI




HOTLINE:+255719050552 +255762198234


Email:mvungi134family@gmail.com

Dodoma,Tanzania

KARIBU UTANGAZE BIASHARA YAKO BEI NI NAFUU
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Blog Archive

My Blog List

Powered by Blogger.