Friday 6 May 2016

Rais Magufuli: Tutagawa Bure Sukari Tutakayo Ikamata Imefichwa na Wafanya Biashara

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewaonya walioficha Sukari na kutishia Kuichukua Sukari hiyo na Kuigawa Bure Kwa Wananchi. Rais Magufuli ametoa onyo kali kwa wafanyabiashara walioficha sukari ili baadae waiuze kwa bei ya juu.

Amesema wafanyabiashara hao wenye tamaa ya pesa walikuwa wakifuata sukari iliyo Expire huko Brazili na kuileta nchini ili watengeneze faida na ndo maana serikali iliwapiga marufuku kuagiza.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akiwasalimia wananchi wa Katesh, Mkoani Manyara. Rais ametoka Mkoani Dodoma leo, anaelekea Mkoani Arusha kwa usafiri wa gari.

Akiongea na mamia ya wananchi hao waliojitokeza kumlaki njiani, Rais Magufuli amewatoa hofu wananchi kuhusu uhaba wa sukari kwa kuwa tayari wako katika mchakato wa kuagiza makontena ya sukari nje ya nchi ili kuwakabili wafanyabiashara walioficha bidhaa hiyo.

Amesema kwa taarifa alizonazo, kuna mfanyabiashara alienda akanunua sukari pale Kilombero zaidi ya tani 3000 na hataki kuzichukua hadi leo

Pia amesema kuna mwingine ana godauni huko Mbagala yenye tani 4000 ambazo hataki kuzitoa ili wananchi wakose sukari.

Rais Magufuli amesema ameviagiza vyombo vya dola viwafuatilie ili ikithibitika sukari waliificha basi ichukuliwe na kugawiwa bure kwa wananchi na pia watapigwa marufuku kufanya biashara yoyote hapa nchini. 

Share:

0 comments:

Post a Comment


Total Pageviews

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

CEO:KOMBO MVUNGI




HOTLINE:+255719050552 +255762198234


Email:mvungi134family@gmail.com

Dodoma,Tanzania

KARIBU UTANGAZE BIASHARA YAKO BEI NI NAFUU
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Blog Archive

My Blog List

  • Happy Christmas - πŸ‘‹πŸ‘ΌπŸ‘‹ Tunawatakia happy Christmas day wadau wetu wa uhakika nakuwa ahidi juu ya kuwapatieni habari za kina katika kila nyanza, halikadhalika similizi ka...
    4 months ago
Powered by Blogger.