WATU
sita wamefariki dunia na wengine nane wamejeruhiwa vibaya katika ajali
iliyohusisha basi dogo la abiria aina ya Hiace lililokuwa likitokea
Mjini Same kuelekea Njoro wilayani Same, ambapo liligongana na gari ya
mizigo aina ya Fuso muda mfupi baada ya kuondoka katika kituo cha abiria
cha Same Mjini.
Daktari aliyezungumza na chanzo cha habari hii katika Hospital ya Wilaya ya Same, Dkt Mlay, amesema wamepokea maiti sita ambazo amebainisha kuwa wanaume ni watano na mwanamke ni mmoja.
Aidha,
ameongeza kuwa Majeruhi nane walipatikana kufuatia ajali hiyo, ambapo
katika Majeruhi hao nane wanawake ni wawili na wanaume sita na kati yao
waliopewa rufaa kuelekea Hospitali ya KCMC -Moshi ni watatu, wanaume
wawili na mwanamke mmoja.
Majeruhi
Noel Bakari Kanumba, aliyekuwa anatokea Mjini Same kwenda Kavambughu,
akizungumza na Mwandishi katika wodi ya Wanaume katika Hospitali ya
Same, amesema alikuwa amekaa kwenye kiti cha mbele na dereva ambapo
aligundua kuwa dereva yule alikuwa amelewa akamwonya asikimbize gari
lakini hakutaka kumwelewa, ndipo gari lilimshinda na kuhama upande wake
na kuelekea upande wa pili na kugonga Fuso upande wa dereva la Fuso hali
iliyosababisha ajali ambapo dereva na abiria wake waliokuwa wamekaa
kiti cha mbele walifariki dunia papo hapo.
Majeruhi
wengine ni Musa Chikira (35), alikuwa anatokea Mjini Same kwenda Njoro
na Mariam Omary Mbaga aliyekuwa katika wodi ya wanawake.
Majerhi wa ajali hiyo, Noel Bakari Kanumba (36), alikuwa anatokea Same Mjini akienda Kavambughu.
Majeruhi wa ajali hiyo, Musa Chikira (35), akiwa amelazwa katika wodi ya wanaume, hospital ya Wilaya ya Same.
Majeruhi wa ajali hiyo, Musa Chikira (35), akiwa amelazwa katika wodi ya wanaume, hospital ya Wilaya ya Same.
0 comments:
Post a Comment