Barakah da Prince na mpenzi wake, Naj.
Juzikati wasanii Baraka Andrew ‘Barakah da Prince’ na Estelina Sanga ‘‘Linah’ walinaswa wakiwa kimahaba, tukio lililoibua gumzo na wengi kudhani mkali huyo wa ngoma ya Siwezi kachepukia kwa ndege mnana.
Barakah da Prince na Linah.
Akilifungukia tukio hilo, Baraka alisema kuwa, yalikuwa ni mapozi ya kawaida tu na wala watu wasihisi anachepuka na Linah.
“Hivi nimsaliti Naj (Najma mpenzi wake wa sasa) sijipendi? Yale ni mapozi ya kawaida tu. Narudia tena, nampenda sana Naj na hakuna mbadala wake,” alisema Baraka.
0 comments:
Post a Comment