Friday, 10 June 2016

HILI NDO JINA LA GOZI JIPYA KWENYE URO 2016

 Kindakindaki cha ligi ya Euro 2016 inaanza  leo nchini Ufaransa ambapo kutakuwa na mchezo mmoja unaohusisha wenyeji Ufaransa watakapambana vikali na Romania katika mchezo utakaopigwa kunako dimba la Stade de France majira ya saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Kama ilivyoada katika michuano ya Ulaya, Amerika na hata dunia kwa ujumla huwa kunakuwa na mpira maalum uliondaliwa kwa ajili ya michunao husika.

Katika michuano ya Euro mwaka huu, mpira utakaotumika unajulikana kwa jina la Adidas Beau Jeu. Beau Jeu ni jina la kifaransa lenye maana ya ‘Beautiful Game’ au ‘Beautiful Play’ ambapo kwa Kiswahili maana yake ni Mchezo mzuri.

Huu ulizinduliwa na Adidas na kutambulishwa na mchezaji wa zamani wa Ufaransa Zinedine Zidane mwezi Novemba mwaka jana.

Mpira huu unajumuisha baadhi ya vitu kama Adidas Brazuca.  Una rangi ya bluu, nyeusi na machungwa huku ukiwa umeandikwa ‘EURO 2016’.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Total Pageviews

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

CEO:KOMBO MVUNGI




HOTLINE:+255719050552 +255762198234


Email:mvungi134family@gmail.com

Dodoma,Tanzania

KARIBU UTANGAZE BIASHARA YAKO BEI NI NAFUU
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Blog Archive

My Blog List

Powered by Blogger.