Sunday 19 June 2016

MDOGO WAKE MWAPE ASAINI RASMI KWA WANAJANGWANI

Obrey akisaini mkataba
Mzambia Obrey Chirwa maarufu kama cholo hatimae ametua rasmi juzi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere na kupokelewa na baadhi ya mashabiki wa Yanga ambao walijitokeza katika uwanja huo. Baada ya kuwasili Obrey alienda moja kwa moja katika makao makuu ya wanajangwani hao mitaa ya twiga na jangwani.

Baada ya kufika alifanikiwa kusaini rasmi kandarasi ya miaka miwili ya kuwatumikia wanajangwani hao maarufu kama wakimataifa. Obrey anakuwa ni Mzambia wa pili kujiunga na wanajangwani hao baada ya Mzambia mwenzake Davies Musonda Mwape aliyeichezea Yanga mpaka 2012 na hatimae kuondoka.
Obrey anaeichezea timu ya taifa ya Zambia chini ya miaka 23 ni mmoja wa washambuliaji wa pembeni hatari wenye chenga za maudhi na anaejua kuzifumania nyavu vilivyo.

amesajiliwa kutokea fc Platinum ya Zimbambwe kwa zaidi ya dola laki moja za kimarekani ambazo ni zaidi ya shilingi milioni mia mbili za kitanzania. Obrey anakuja kuchukua nafasi ya Mniger Isofou Aboubaca ambaye amesitisha mkataba na wanajangwani hao baada ya kutoridhishwa na kiwango chake.

Cholo anakuja kuungana na Donald Ngoma na Thabani Kamusoko ambao walicheza pamoja fc Platinum, kombinesheni ya Ngoma Tambwe na Obrey inategemewa kuja kuisaidia Yanga katika mashindano yanayoendelea hivi sasa ya kombo la shirikisho amabayo leo Yanga wanacheza na FC Mo Bejaia ya Algeria majira ya saa 6;45 usiku.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Total Pageviews

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

CEO:KOMBO MVUNGI




HOTLINE:+255719050552 +255762198234


Email:mvungi134family@gmail.com

Dodoma,Tanzania

KARIBU UTANGAZE BIASHARA YAKO BEI NI NAFUU
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Blog Archive

My Blog List

  • Happy Christmas - πŸ‘‹πŸ‘ΌπŸ‘‹ Tunawatakia happy Christmas day wadau wetu wa uhakika nakuwa ahidi juu ya kuwapatieni habari za kina katika kila nyanza, halikadhalika similizi ka...
    8 months ago
Powered by Blogger.