Thursday, 30 June 2016

MZIGO WA KODI KUBWA WAANZA LEO RASMIII

Dar es Salaam. Leo ndiyo mwanzo wa utekelezaji wa Sheria Fedha (Finance Act, 2016) iliyopitishwa katika Bajeti ya 2016/17 na Kodi ya Ongezeko la Thamani (Vat) itatozwa kwa huduma za mitandao ya simu, benki na taasisi za fedha.

Akisoma hotuba ya bajeti bungeni hivi karibuni, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango licha ya mambo mengine, alipendekeza kuongeza kodi hiyo katika huduma za benki zinazotozwa ili kupanua wigo wa kodi isipokuwa riba kwenye mikopo.

Vilevile, Waziri Mpango alieleza azma ya Serikali kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia 10 kwenye ada zinazotozwa na watoa huduma katika kutuma na kupokea fedha badala ya ushuru huo kutozwa tu kwenye kutuma fedha pekee.

Akizungumzia uamuzi huo, mtaalamu wa kodi wa kujitegemea, Deogratias Peter alisema ongezeko hilo litawakatisha tamaa wateja wa benki na watumiaji wa miamala ya simu.
Share:
Share:

0 comments:

Post a Comment


Total Pageviews

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

CEO:KOMBO MVUNGI




HOTLINE:+255719050552 +255762198234


Email:mvungi134family@gmail.com

Dodoma,Tanzania

KARIBU UTANGAZE BIASHARA YAKO BEI NI NAFUU
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Blog Archive

My Blog List

Powered by Blogger.