Chuo
cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kimesikitishwa na habari zilizochapishwa
na gazeti la RAI Toleo la 1249 la tarehe 5 – 11 Mei 2016 ambazo ni za
upotoshaji.
Tunapenda
kufafanua kuwa taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) zinaeleza kuwa, Chuo cha Usimamizi wa Fedha kilipokea
fedha za ziada kutoka Wizara ya Fedha kwa ajili ya mishahara na fedha
hizo zilishapangwa kurudishwa ndani ya mwaka wa fedha 2015/2016 kama
ripoti ya Mkaguzi ilivyoagiza katika mwaka wa fedha wa 2014/2015. Kwa
hiyo fedha hizo hazijatafunwa wala kupotea.
Kuhusu
ukusanyaji wa madeni yaliyoripotiwa, nusu ya deni ni karo ya wanafunzi
wanaolipiwa na Bodi ya Mikopo na fedha hiyo ililipwa Chuoni ndani ya
mwaka wa fedha 2014/2015.
Madeni
mengine ni ya wanafunzi walioshindwa kuendelea na masomo kwa sababu
mbalimbali na madeni hayo yanafutwa kwa kufuata taratibu za kifedha
(Financial Regulation) kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za
serikali alivyoelekeza.
Ufanunuzi
huu ulitolewa kwa mwandishi wa gazeti hili (Bwana Gabriel Mushi) mnamo
tarehe 04-05-2016 alipoongea na Naibu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na
Utawala.
Kwa
kumalizia Chuo cha Usimamizi wa Fedha kinafanya kazi zake kwa kufuata
taratibu zilizowekwa na kwa zaidi ya miaka 30 mfululizo Chuo kimepata
hati safi za mahesabu (Clean Audit Report) kwa mujibu wa Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG).
0 comments:
Post a Comment