Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo leo imetangaza kumfungia Snura kujihusisha na masuala ya sanaa.
Pia
imeufungia wimbo wake Chura pamoja na video yake kutochezwa kwenye
redio na TV nchini. Taarifa hiyo imetolewa na wizara hiyo kwenye mkutano
na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wake wa mikutano
wizarani hapo jijini Dar.
Uamuzi wa kumfungia umekuja kutokana msanii huyo kutojisajili kwenye Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA.
Akiongea
na waandishi wa habari, Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa wizara hiyo,
Zawadi Msalla, amewaonya watu kutousambaza wimbo huo kwenye mitandao ya
kijamii ikiwemo WhatsApp.
0 comments:
Post a Comment