leo Alfajiri katia mechi ya kukata nashoka baina ya Argentina na Chile kwenye michuano ya COPA AMERICA inayorindima kunako bara la
Marekani.
Argentina walijipatia bao la kwanza dakika ya 50 kupitia kwa
mshambuliaji wa pembeni anayekipiga kunako klabu ya PSG, Angel Di Maria,
dakika 9 baadaye Chile walifanya chambulio la nguvu langoni mwa
Argentina lakini halikuzaa goli na papo hapo Argentina wakatumia mwanya
huo kufanya 'Counter Attack' langoni mwa Chile na bila ajizi Ever Banega
akatumbukiza bao la pili, na kufanya ubao wa matokeo kusomeka 2-0.
Katika dakika za majeruhi Jose Fuenzalida akaipatia Chile bao la kufutia
machozi. Mwisho wa mchezo Argentuna 2, Chile 1.
Kwenye kipute cha awali kwa siku hii kilichopigwa ndani ya dimba la Levs
jijini Califonia, Panama iliifunga Bolivia kwa mabao 2-1,washindi
walianza kujipati bao kupitia kwa mchezaji Alberto Quintero's kunako
dakika ya 10 tu ya mchezo alipounganisha kwa mtindo wa "slide motion"
krosi ya Blas Perez,bao lililodumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili Bolivi walijipapatua na kusawazisha bao kupitia kwa
Juan Carlos Arce baada ya mabeki wa Panama kuzubaa kuuondoa mpira
langoni mwao.Kunako dakika ya 87 Panama walihanikiza ushindi kwa
kupachika bao la pili lililofungwa na mshambulizi Blas Perez.
Leo ni
MAREKANI vs COSTA RICA
COLOMBIA vs PARAGUAY
0 comments:
Post a Comment