MAMLAKA YA HALI YA HEWA (TMA) YATOA MWELEKEO WA HALI YA HEWA KWA KIPINDI CHA JUNI HADI AGOSTI 2016.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa mwelekeo wa
hali ya hewa kwa kipindi cha Juni hadi Agosti mwaka huu. Akizungumzia
kuhusiana na mwelekeo huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Meneja Kituo
Kikuu cha Utabiri Bw. Samwel Mbuya alisema “Nchi yetu inatarajia kuwa na
hali ya baridi kiasi katika kipindi hiki sambamba na vipindi vifupi vya
mvua vinavyotarajiwa kujitokeza katika maeneo machache hususanya ukanda
wa Ziwa Viktoria na ukanda wa pwani ya Kaskazini (Visiwa vya Unguja na
Pemba).
Katika kipindi cha mwezi Juni hadi Agosti 2016, maeneo mengi ya nchi
yanarajiwa kuwa makavu na yenye hali ya baridi kiasi katika majira haya
ya kipupwe. Mifumo ya hali ya hewa inaonesha matarajio ya hali ya joto
la wastani hadi chini ya wastani katika maeneo yaliyopo Kusini-magharibi
mwa nchi.
Hata hivyo,katika msimu wa Kipupwe wa mwaka huu maeneo mengi ya nchi
yanatarajiwa kuwa na joto la wastani hadi juu ya wastani. Aidha,
izingatiwe kuwa hali ya ubaridi inatarajiwa zaidi nyakati za usiku hadi
mapema asubuhi. “Aliendelea kueleza sababu za hali hiyo kuwa ni pamoja
na kupungua kwa joto la bahari katika eneo la ukanda wa Tropiki la
bahari ya Pasifiki sambamba na Joto la baharà katikaeneo la magharibi wa
bahari ya Hindi kuwa la wastani kwa kipindi cha miezi ya Juni hadi
Agosti 2016”.
Aidha, joto katika bahari ya Atlantiki linatarajiwa kuwa chini ya
wastani. Hali hiyo inatarajiwa kusababisha upepo kuvuma kutoka magharibi
ukielekea mashariki hususankatika maeneo ya Ukanda wa Ziwa Viktoria.
Joto la bahari la juu ya wastani linatarajiwa katika eneo la ncha ya
kusini ya bara la Afrika hivyo kuathiri msukumo wa upepo wa kusi.
Kwa upande mwengine, Afisa Uhusiano wa TMA, Bi. Monica Mutoni alitoa
msisitizo kwa wananchi kufuatilia taarifa hususan za tahadhari
zinazotolewa na Mamlaka kupitia vyombo mbalimbali vya habari, tovuti ya
Mamlaka n.k ili kuokoa maisha na mali. Bi. Monica alisema “Hivi karibuni
TMA imekuwa ikitoa tahadhari mbalimbali ikiwa ni pamoja na za kuwepo
kwa upepo mkali na mawimbi makubwa kwenye ukanda wa Bahari Hindi, Maziwa
na nchi kavu hivyo ni vyema wananchi hasa wale watumiaji wa bahari na
maziwa kuchukua hatua stahiki pindi taarifa kama hizo zinapotolewa”.
Aidha, TMA ilipongeza sekta mbalimbalipamoja na Taasisi, Mamlaka za
Serikali na jamii kwa ujumla kwa hatua stahiki zilizochukuliwa katika
kipindi chamsimu wa mvua za Masika 2016 kwa kutumia Taarifa, Agalizona
Tahadhari za utabiri zilizotolewa na Mamlaka. Ni wazi kuwa kwa hatua
hizo madhara ambayo yangeweza kujitokeza yalidhibitiwa na hivyo
kuchangia katika kufanikisha mipango na utekelezaji wa shuguli za
kiuchumi na kijamii katika kipindi husika.
Kwa tarifa ya kina kuhusiana na mwelekeo wa hali ya hewa kwa mkoa wako
ingia kwenye tovuti ya TMA www.meteo.go.tz au tembelea ofisi zetu
IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Meneja wa Kituo Cha Utabiri Kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
(TMA) Bw. Samwel Mbuya akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Jijini Dar
es salaam kuhusu mwelekeo wa Hali ya joto na mvua katika kipindi cha
juni hadi Agosti 2016 ambapo inatarajiwa kuwa na hali ya baridi kiasi na
vipindi vifupi vya mvua. Kulia ni Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Bi
Monica MutoniBaadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)na vyombo vya Habari Leo Jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment