YOUNG KILLER AMTOLEA POVU NGOSHA
Young Killer alisema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Planet Bongo
ya East Africa Radio na kusema yeye anawakubali sana Nikki Mbishi,
Godzilah pamoja na marehemu Albert Mangwea kwa kufanya ‘Free style’
sababu anatambua uwezo wao katika nyanja hiyo.
“Sijawahi kumkubali Fid Q kwa ‘free style’ sababu
sijawahi kumuona akifanya hivyo ila niliowahi kuwaona wakifanya mitindo
huru nampenda sana Nikki Mbishi, GodZillah pamoja marehemu
Albert Magwea” alisema Young Killer
Mba na hilo Young Killer amesema baada ya kufanya kazi na Fid Q
msanii mwingine wa hip hop anayetamani kufanya naye kazi kwa sasa ni
Mbunge wa mikumi ‘Prof Jay’.
“Kiukweli kabisa kwa sasa hivi mimi natamani sana kufanya
kazi na Prof Jay, hata hivyo tayari nipo kwenye mipango ya kufanya kazi
na rapper Chemical “. Aliongeza Young Killer.
eatv.tv
0 comments:
Post a Comment