Taarifa kutoka Ikulu ya Tanzania leo
June 26 inasema Rais John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko kwenye
nafasi za wakuu wa Mikoa pamoja na wakuu wa Wilaya,kwenye mabadiiko hayo
amewateua jumla ya wakuu wa wilaya 139.
Mabadiliko haya yanamhusu aliyekua mkuu wa Wilaya ya Sengerema
Bi.Zainab R. Telack kuwa mkuu mkoa wa Shinyanga ambaye anajaza nafasi
iliyoachwa wazi na aliyekua mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi.Anna Kilango
Malecela.Mwingine aliyehusishwa na mabadiliko haya ni pamoja na Dkt Binilith Satano Mahenge kuwa mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Dkt. Satano anajaza nafasi ilyoachwa wazi na aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam ambapo atapangiwa majukumu mengine.
Mwingine aliyeteuliwa ni Dkt. Charles F Mlingwa ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Mara na anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw.Stanslaus Magesa Mulongo ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Nimeipata pia List ya wakuu wa Wilaya wapya mtu wangu nimekuwekea na List ya wilaya zao.
0 comments:
Post a Comment