Wednesday, January 25, 2017
Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kutia saini sheria kuweka masharti kuhusu wahamiaji wanaoingia nchini humo.
Taarifa
kutoka Marekani zinasema ataanza kwa hatua ya kuimarisha usalama katika
mpaka wa nchi hiyo na Mexico atakapozuru makao makuu ya wizara ya
usalama wa ndani leo Jumatano.
Aidha,
anatarajiwa pia kutoa tangazo la kuidhinisha sheria kali zaidi za
kupata visa kwa wageni kutoka eneo la Mashariki ya Kati na Afrika ambayo
yana Waislamu wengi
Bw Trump ameandika kwenye Twitter kwamba leo itakuwa siku muhimu sana kwa usalama wa taifa la Marekani.
Wakati wa kampeni yake ya urais, Donald Trump aliahidi kufanyia mageuzi suala la uhamiaji Marekani.
Aligusia
ujenzi wa ukuta kati ya Mexico na Marekani kuzuia wahamiaji haramu na
kuwapiga marufuku Waislamu kuingia katika taifa hilo kama sehemu ya vita
dhidi ya ugaidi.
Baadaye alibadili msimamo kidogo na kufafanua kwamba watakachofanyiwa Waislamu ni kufanyiwa ukaguzi mkali kabla ya kuruhusiwa kuingia Marekani.
Baadaye alibadili msimamo kidogo na kufafanua kwamba watakachofanyiwa Waislamu ni kufanyiwa ukaguzi mkali kabla ya kuruhusiwa kuingia Marekani.
Anatarajiwa
kufika katika wizara ya usalama wa ndani baadaye leo na anatarajiwa
kusaini maagizo hayo ya kuimarisha usalama katika mpaka wa Mexico na
taifa lake na baadaye wiki hiii taarifa zinaashiria atawajibikia ahadi yake ya kupunguza idadi ya wakimbizi wanaoingia Marekani.
Na
hiyo ni hadi pale ukaguzi mkali utakapoanzishwa na kuzuia raia wa
mataifa saba ya Afrika na kutoka eneo la Mashariki ya Kati yote yalio na
idadi kubwa ya waumini wa Kiislamu.
Ubaguzi
wa kidini unapigwa marufuku kwa mujibu wa katiba ya Marekani lakini
inadhaniwa utawala wa Trump utaidhinisha marufuku hiyo kwa misingi
kwamba ni hatua za dharura kukabiliana na tishio lililopo la ugaidi.
Awali,
Bw Trump aliandika kwenye Twitter kueleza kusikitishwa kwake na kiwango
cha juu cha ghasia na mauaji katika jiji la Chicago.
Vyombo vya habari wiki hii viliripoti kwamba tayari watu 228 wamepigwa risasi na wengine zaidi ya 40 kuuawa mwaka huu.
Bw
Trump ameandika kwamba iwapo watawala wa Chicago hawatatua tatizo hilo
la mauaji, basi atawatuma 'Feds' akimaanisha maafisa wa FBI.
Chanzo: BBC
Chanzo: BBC
0 comments:
Post a Comment