Tuesday 14 June 2016

HAYA NDO MAMBO YANAYO HATARISHA MAISHA



Kufanikiwa au kutokufanikiwa kwa mwanadamu huwa kunatokana na mchango wa mambo mengi. Mambo hayo huwa yapo ambayo wengine wanayajua na pia wengine hawayajui kabisa. Lakini kwa kifupi, huwa yapo mambo yanayoathiri maisha yetu iwe kwa chanya au hasi ilimradi tu ukikutana nayo.
Kutokana na athari hizo zinazotokana na mambo hayo, hiyo inatuthibitishia kwamba maisha uliyonayo yapo hivyo kutokana na athari ulizozipokea, ambazo zinaweza zikawa chanya au hasi. Kwa kusoma makala haya, utajifunza mambo muhimu yanayo athiri maisha na malengo yako kwa ujumla. Je, mambo hayo ni yapi?
1. Mazingira.
Mazingira tunayoishi yana mchango mkubwa sana katika kutengeneza au kuharibu maisha ya mtu. Kwa mfano ukiwa umezaliwa na kukulia katika mazingira ya umaskini ni ngumu sana kwako kuamini kama ipo siku unaweza kuwa tajiri. Halikadhalika, unapokuwa umekulia katika mazingira ya familia tajiri ni rahisi sana kuamini ni lazima na wewe tajiri.
Tambua, mazingira yoyote uliyopo yana mchango mkubwa sana kwenye maisha yako, haijalishi huo mchango ni hasi au chanya. Kikubwa jifunze kuyatumia mazingira uliyonayo yakusaidie kufanikiwa hata kama ni mabaya. Kama upo kwenye mazingira yanakurudisha nyuma unatakiwa kutoka hapo haraka sana kwa kujitengenezea mazingira chanya ya kukusaidia kufanikiwa.


2. Matukio.
Hakuna ubishi pia matukio yana uwezo mkubwa wa kuathiri maisha yetu kwa kiasi kikubwa. Haijalishi matukio hayo ni hasi au chanya lakini yanauwezo wa kuathiri maisha yako. Unaweza ukawa umeanza kujiuliza matukio kama yapi yana uwezo wa kuathiri maisha yangu? Tulia kidogo nikupe mfano wa kukusaidia kunielewa katika hili vizuri kabisa wala usiwe na haraka.
Kwa mfano unapokabiliana na matukio kama afya mbovu, kufiwa mara kwa mara au ajali, kwa matukio haya ni rahisi sana kukufanya ukaona dunia mbaya na sehemu ambayo siyo sahihi kwako. Pia unapokutana na matukio kama ya kushinda kitu fulani au kufanikiwa, matukio hayo yanapofatana  yanauwezo mkubwa kukujengea kujiamini na kuathiri maisha na malengo yako kwa ujumla. 
3. Maarifa.
Naamini sote tunajua hakuna kitu kibaya na ambacho kina uwezo wa kukukosesha mafanikio kama kukosa maarifa. Nguzo kubwa ya mafanikio imejikita kwenye maarifa. Watu wote wenye mafanikio, wana maarifa sahihi ya kuwasaidia kufanikiwa. Kutokuwa na maarifa ya kuweza kukusaidia kwenye maisha ni kama ujinga fulani hivi.
Watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwa sababu ya kukosa maarifa muhimu ya kuwasaidia kufanikiwa. Wengi hawako tayari kutoa ujinga ulio kichwani mwao kwa kujifunza, zaidi hubaki kama walivyo. Kwa kawaida,  unapokuwa na maarifa bora ni rahisi kufanikiwa, lakini unapokuwa huna maarifa sahihi kufanikiwa inakuwa sio rahisi kabisa.
4. Matokeo.
Jambo lingine linaloweza kuathiri maisha na malengo yetu ni matokeo. Mara nyingi sana tunaathiriwa na matokeo, iwe matokeo yetu binafsi, matokeo ya kijamii au ya kifamilia. Kwa mfano tunapokuwa tuna matokeo mabaya kwa mfululizo yawe ya kifedha, mahusiano mabaya na jamii au kifamilia matokeo hayo ni rahisi sana kuharibu maisha yetu kwa kuamini hiyo ndiyo sehemu ya maisha yetu.
Lakini matokeo yanapokuwa mazuri hiyo hutusaidia sana kujiamini na kujikuta tunatengeneza maisha yetu na kuwa bora zaidi. Hivyo, kwa namna yoyote ile matokeo yanamchango mkubwa wa kuathiri maisha yako. Jaribu kuangalia ni matokeo gani ambayo umekuwa ukiyapata mara kwa mara? kwa matokeo hayo elewa  yanauwezo kuharibu au kujenga maisha yako.  
 5. Ndoto zetu.
Wakati mwingine maisha na malengo yetu yanaathiriwa sana na ndoto tulizonazo. Kutokana na udogo wa ndoto tulizonazo hupelekea kuishi maisha mabaya ama kutokana na ukubwa wa ndoto tulizonazo hupelekea kuishi maisha ya mafanikio. Kitu cha kujiuliza ndoto ulizonazo ni zipi? Kwa ndoto zozote ulizonazo, zina uwezo wa kuathiri maisha na malengo uliyonayo.
Kwa kifupi, mazingira, matukio, maarifa na ndoto zetu tulizonazo, ni baadhi ya mambo yenye uwezo wa kuathiri maisha na malengo yetu kwa sehemu kubwa sana kuliko tunavyofikiri.
Nikutakie siku njema na kila la kheri katika safari ya kufikia mafanikio makubwa.
Kwa makala nyingine za mafanikio jifunze pia kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Share:

0 comments:

Post a Comment


Total Pageviews

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

CEO:KOMBO MVUNGI




HOTLINE:+255719050552 +255762198234


Email:mvungi134family@gmail.com

Dodoma,Tanzania

KARIBU UTANGAZE BIASHARA YAKO BEI NI NAFUU
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Blog Archive

My Blog List

  • Happy Christmas - πŸ‘‹πŸ‘ΌπŸ‘‹ Tunawatakia happy Christmas day wadau wetu wa uhakika nakuwa ahidi juu ya kuwapatieni habari za kina katika kila nyanza, halikadhalika similizi ka...
    8 months ago
Powered by Blogger.