Picha
chafu z i l i z o v u j a zikimuonesha Video Queen wa Bongo, Agness
Gerald ‘Masogange’ akiwa kihasarahasara na mwanaume anayesemekana ni
msanii wa Bongo Fleva, Regnald Raymond ‘Reggy’ zimeibua hasira kwa
mpenzi wake ambaye ni mwigizaji wa Bongo Muvi, Rammy Galis na kutishia
kuvunja penzi lao.
Chanzo
chetu makini kabisa kilisema kuwa ingawaje inadaiwa kuwa picha hizo ni
moja ya kurekodi nyimbo inayoitwa Kampa Kampa Tena ya mwanamuziki huyo
lakini baadhi ya picha zilizovuja ni chafu na haziko kwenye video ya
wimbo huo kitu ambacho kilizidi kuwapa maswali watu mbalimbali ya kuwa
kuna kitu kingine zaidi ya picha hizo.
“Sawa
wao wenyewe wanasema kuwa ni vipande vya picha vilivyopo kwenye video
ya nyimbo hiyo lakini kwenye nyimbo hiyo ukiitazama vipande hivyo
havionekani kabisa,” kilidai chanzo hicho. Mpashaji wetu huyo aliendelea
kufunguka kuwa baada ya picha hizo kuvuja mpenzi wa sasa wa Masogange
inadaiwa alimpigia simu kijana huyo na kumpa kashikashi huku
akimtaka aache kusambaza picha hizo la sivyo wasije kulaumiana.
Gazeti
hili lilipoinyaka habari hiyo lilimtafuta kwanza mwanamuziki huyo
ambapo alikana kuwa yeye si mwanzilishi wa kusambaza picha hizo kwa
sababu hakuwa na sababu ya kufanya hivyo.
Rammy
Galis alipotafutwa kuzungumzia jinsi picha hizo zilivyomchefua hakuweza
kupatikana mara moja. Hata hivyo, Masogange alipotafutwa kupitia simu
yake ya mkononi alisema: “Unajua kila kukicha watu wanapenda kuibua
mambo, ile ni video na mpenzi wangu anaijua, kama kuna kutofautiana na
mpenzi wangu picha hizo wala siyo sababu.”
0 comments:
Post a Comment