Sunday, February 26, 2017
Mbunge Paulina Gekul anusurika Kifo......Alazwa ICU, Ziara yaahirishwa
Mbunge
wa jimbo la Babati mjini Paulina Gekul nusra kupoteza maisha yake baada ya gari
lake lenye namba za usajili T 189 BHQ kupata ajali.
Inasemekana chanzo cha ajali hiyo ni gari kuacha njia na kupinduka vibaya
ambapo mbunge huyo alikuwa katika msafara wa naibu waziri wa Mazingira
Luhaga Mpina wilayani Babati mkoa wa Manyara.
Baada
ya ajali hii kutokea mmbunge Paulina Gekul ambaye ni mmbunge wa babati
mjini akakimbizwa hospitali ya mkoa wa manyara na kulazwa katika chumba
cha wagonjwa mahututi I.C.U huku wanahabari wakikatazwa kuingia katika
chumba hiki na madakatari ambao wanamuhudumia mbunge huyo
Hata
hivyo baada ya ajali kutokea naibu waziri wa mazingira amelazimika
kuahirisha ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya mji wa
babati huku mpina akiipongeza halmasahauri ya mji wa babati kwa kutambua
umuhimu wa kutunza mazingira katika hali ya usafi baada ya kununua gari
kwaajili ya kubebea taka lenye thamani ya zaidi ya milioni 200.
NA MVUNGI K.A
0 comments:
Post a Comment