Msani wa bongo fleva Nay wa mitego atangaza nia yake ya kuanzisha kanisa takatifu.
Anadai kua kanisa lake halitakua la upigaji wa mkwanja kama makanisa feki yanavyofanya.
“Acha
kanisa likamilike, mwenye Mungu asimamie tutajua nini kinaenda kutokea
lakini sio kanisa kwaajili ya kupiga hela,” Nay aliiambia E-News.
Nay
amedai kuwa mchungaji wa kanisa lake atakuwa tofauti na hatotegemea
sadaka za waumini ili kuendesha maisha yake, bali kazi yake nyingine
itakayoweza kumuingizia kipato.
Rapper
huyo amejinadi kuwa anatarajia kupata waumini wengi kupitia kanisa lake
na kwamba litakuwa chanzo cha mafanikio katika mambo yao.
Nay amedai kuwa kanisa lake litajengwa Mbezi ya Kimara jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment