Tuesday, 14 June 2016

Daah! LIL WYNE ANAUGUA KIAFAFA, jioneee

Rapper machachari na mtalamu wa kuflow kwa makeke lil wayne amesumbuliwa tena na kaugonjwa kake ka kuanguka kifafa.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, ndege binafsi aliyokuwa amepanda rapper huyo, ililazimika kutua kwa dharura huko Omaha, Nebraska Jumatatu hii. Weezy alikuwa akisafiri kutoka Milwaukee kwenda California pindi tukio hilo lilipotokea.

Wayne alidaiwa kuzimia akiwa kwenye ndege na kupewa huduma ya kwanza. Hata hivyo ripoti zimedai kuwa alikataa kutibiwa. Taarifa zimedai kuwa alipata tena kifafa cha pili baada ya ndege yake kupaa na ililazimika arudishwe Omaha. Alipoteza kabisa fahamu na alipelekwa hospitali kwa ambulance.

Tunechi aliwahi kupata tatizo kama hilo mwaka 2012 baada ya ndege binafsi kutua kwa dharura kwa siku mbili mfululizo. Pia aliwahi kupata kifafa kikali mwaka 2013.

Share:

0 comments:

Post a Comment


Total Pageviews

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

CEO:KOMBO MVUNGI




HOTLINE:+255719050552 +255762198234


Email:mvungi134family@gmail.com

Dodoma,Tanzania

KARIBU UTANGAZE BIASHARA YAKO BEI NI NAFUU
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Blog Archive

My Blog List

Powered by Blogger.