- Kiungo wa zamani wa African Sports, Coastal Union na Simba SC, Ibrahim Twaha ‘Messi’ ameamua kuichagua Mtibwa Sugar ya Turiani, Morogoro na kusaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu.
Twaha anayetumia mguu wa kushoto lakini akiwa hatari katika mashambulizi akitokea upande wa wing ya kulia ameithibitishia www.shaffihdauda.co.tz kujiunga kwake na Mtibwa akitokea Coastal iliyoteremka daraja.
“Nitaichezea Mtibwa Sugar msimu ujao baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu”, anasema Twaha nilipofanya naye mahojiano mapema Alhamis hii.
“Nimeichagua Mtibwa kwa sababu ni timu iliyokuwa ikinihitaji sana hata kabla ya kujiunga na Simba (2013.) Kila wakati wa usajili ukifika, kocha Mecky (Mexime) amekuwa akinitaji. Ni sehemu nzuri.”
Kumsaini Twaha kumeendeleza tabia ya kocha Mecky Mexime kuwasaini wachezaji vijana. Mtibwa tayari imempoteza mlinzi wake wa kati Vicent Andrew aliyejiunga na Yanga na kocha huyo kijana amesema hana tatizo ikiwa nyota wake watasajiliwa na klabu nyingine.
Mzee Philemon Ndesamburo afariki dunia
-
Wednesday, May 31, 2017
Breaking News: Mzee Philemon Ndesamburo(CHADEMA) afariki dunia
Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini (Chadema) Philemon Ndesamburo...
7 years ago
0 comments:
Post a Comment