Yanga imefuzu kwa nane bora ya michuano ya CAF kwa mara ya nne huku ikiwa ni mara yao ya kwanza kufika hatua hiyo katika Confederation Cup. Chini ya wakufunzi, Hans Van der Pluijm, Juma Mwambusi na Juma Pondamali.
Kikosi hicho kilichotwaa kwa mara ya pili mfululizo ubingwa wa ligi kuu mwezi Mei kimeingia kambini kikiwa na wachezaji wake wapya, Hassan Kessy, Juma Mahadhi na Vicent Andrew ambao wamejiunga na timu hiyo wakitokea klabu za Simba SC, Coastal Union na Mtibwa Sugar.
Yanga itaanza kucheza ugenini Juni 17 imepanga kuweka kambi ya wiki moja nchini Uturuki kabla ya kutua nchini Algeria kusaka ushindi wa kwanza wa kihistoria katika ‘ardhi ya Mwarabu.’
“Tayari tumeanza kambi ya maandalizi kuelekea michuano ya CAF wiki hii na wachezaji wote tayari wameshawasili na kuanza mazoezi.” anasema mkuu wa kitengo cha habari wa klabu hiyo Jerry Murro.
“Amis Tambwe na Donald Ngoma hawakuonekana katika mazoezi ya kwanza lakini tayari wameshawasili. Kutokana na sababu za kimazingira, kule walipotoka hadi kufika Dar es Salaam tumeona wapumzike kwanza lakini wataanza mazoezi wiki hii.”
“Tunategemea kuweka kambi ya wiki moja nchini Uturuki au tunaweza kuondoka kutoka hapa hadi Algeria kwa ajili ya mchezo. Itategemea ratiba ya ndege na urahisi wa kufika Algeria. Bado tupo katika mazungumzo na mashirika ya ndege na tutawaambia kitakachojiri kwa maana ni lazima tufanye hivyo.”
Kwa ukaribu zaidi, tafadhali unaweza ku-LIKE PAGE yangu BSports. Utapata Updates za michuano mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment