MWANAMITINDO na Mtangazaji wa Kipindi cha Keeping Up With The
Kardashians, Kim Kardashian hivi karibuni alimfanyia sapraizi shabiki
wake baada ya kumzawadia kiatu toleo la Yeezy Boost 750 chenye thamani
ya shilingi laki saba za Kibongo.
Mwanadada Kim ambaye ni mama wa watoto wawili aliozaa na mumewe ambaye ni rapa, Kanye West aliandika katika ukurasa wake wa twitter.
“Vema, leo imekuwa bahati kwako… Saizi ipi inakufaa, nimekutafutia namba 10! Msaidizi wangu atawasiliana chemba na wewe kupata mawasiliano yako na Yeezy itasafirishwa kwako.”
Kiatu cha Yeezy Boost 750 bado hakijatoka, kitatoka Juni 11, mwaka huu na Kim aliweka tangazo kwenye Twitter yake kama hamasa kwa mashabiki kwa mtu atakayetoa ‘posti’ bora ya kukitangaza.
Yeezy Boost 750

0 comments:
Post a Comment