Najua mashabiki na wanachama wa Yanga wote walikuwa wanasubiri kwa hamu kujua matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu wa Yanga katika nafasi mbalimbali, hususani ya mwenyekiti na makamu wake.
Katika nafasi ya mwenyekiti Yusuph Manji ndio
alikuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo, kura za awali zimetangazwa yeye
amepata jumla ya kura za ndio 1468, hapana 0 na kura mbili ndio
zimeharibika.
Kwa upande wa nafasi ya makamu mwenyekiti Clement Sanga amepata jumla ya kura 1428 wakati mpinzania wake Ossoro amepata jumla ya kura 80, matokeo rasmi ya uchaguzi mkuu wa Yanga yatatangazwa kesho Jumapili ya June 12 2016.
NA MVUNGI K.A
0 comments:
Post a Comment