Forbes wametoa
list ya wanamichezo 100 matajiri duniani, kwa upande wa TOP 10 mchezo
wa soka ambao ndio unatazamiwa kuwa unaingiza hela nyingi, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi pekee ndio wamefanikiwa kuwa na utajiri uliowafaya waingie TOP 10.
Ronaldo ndio
ameongoza katika list ya wanamichezo matajiri duniani kwa kuwa na
utajiri wa dola milioni 88 ambazo ni zaidi ya bilioni 190 za kitanzania,
Lionel Messi ameshika nafasi ya pili kwa kuwa na utajiri wa dola milioni 81.4 ambazo ni zaidi ya bilioni 178 za kitanzania.
Cristiano Ronaldo utajiri
wake wa dola milioni 32 ambazo ni zaidi ya bilioni 70 za kitanzania
unatokana na mikataba ya matangaza kupitia account zake za social
network kama twitter, instagram na facebook.
0 comments:
Post a Comment