Maria Sarapova ni miongoni mwa wanawak matajiri duniani, ambaye ni mcheza tennis maarufu. Maria Sharapova ameitikisa wimbi la michezo duniani baada ya kufungiwa kucheza Tennis kwa muda
wa miaka miwili, na hii ni mara tu baada ya kunaswa na vipimo vya kisasa juu ya kile kinacho itwa utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu.
Shirikisho la Tennis la kimataifa duniani (ITF) limemfungia Maria Sharapova baada ya kugundua kuwa amekuwa akitumia dawa hizo za kusisimua misuli aina ya Meldonium kwa muda mrefu.
Shirikisho hilo limetangaza rasmi June 8 2016 kuwa mrembo huyo hatoruhusiwa kucheza tennis kwani amekiuka sheria za michezo, ingawa imetangazwa rasmi kufungiwa kwake, Maria Sharapova anasema yeye amekuwa akitumia dawa hizo kwa matibabu ya moyo tangu mwaka 2006.
0 comments:
Post a Comment