Tuesday, 21 June 2016

MZEE WA MIAKA 65 AMTIA MIMBA BINTI WA MIAKA 16

Hai. Mzee  wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Nkuu Kisereny mwenye umri wa miaka 65  amempa ujauzito binti mwenye umri wa miaka 16 ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Nkuu iliyopo maeneo ya Machame wilaya ya Hai.

Hali hiyo imezua taharuki baada ya wananchi wenye hasira kali, hususani wazee kujitoa kumtafuta mtuhumiwa, huku wakidai kuwa wamechoshwa na vitendo vyake vya kuwarubuni mabinti wadogo kwa kuwapatia vizawadi vidogovidogo.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Ndelilio Mwenda alisema binti huyo alibainika kuwa na ujauzito wa miezi sita baada ya upimaji kufanyika katika moja ya zahanati zilizopo Machame na  alipohojiwa alimtaja mzee huyo ambaye alisema ni mjomba wake.

“Kama ilivyo kawaida agizo la upimaji mimba kwa wanafunzi hufanyika kila mara na ni agizo la lazima kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa,”alisema Mwenda.Search
Share:

0 comments:

Post a Comment


Total Pageviews

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

CEO:KOMBO MVUNGI




HOTLINE:+255719050552 +255762198234


Email:mvungi134family@gmail.com

Dodoma,Tanzania

KARIBU UTANGAZE BIASHARA YAKO BEI NI NAFUU
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Blog Archive

My Blog List

Powered by Blogger.