Chama cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Serikali kumpiga marufuku Katibu
Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kuhudhuria
hafla na matukio ya kitaifa kutokana na kitendo alichokifanya hivi
karibuni kwenye msiba wa Rais wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Aboud Jumbe.
Maalim Seif alikataa kumpa mkono Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed
Shein kufuatia msimamo wa chama hicho wa kutoshirikiana na Serikali
Visiwani humo, wakipinga kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba
25 na Kufanyika kwa Uchaguzi wa Marudio uliompa ushindi wa kishindo Dkt.
Shein baada ya CUF kuususia.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai alisema kuwa ni
muda muafaka sasa kwa Serikali kumzuia kushiriki matukio ya kitaifa.
Alisema CCM imefadhaishwa na kitendo alichokifanya Maalim Seif na
kuwataka watu wote kukilaani.
“Nawaomba watu wasiendekeze sakata hili kwa sababu linamdhalilisha
Maalim,” alisema Vuai. “Hatukutarajia kiongozi kama Maalim kufanya
kitendo kama kile,” aliongeza.
Hili ni tukio la kwana kwa Maalim kugoma kumsalimia Dkt. Shein.
Awali, Dkt. Shein alimtembelea Maalim Seif na kumjulia hali katika hotel
ya Serena jijini Dar es Salaam na walizungumza vizuri wakiombeana heri.
0 comments:
Post a Comment