Siku kadhaa
baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kusema kuwa hawezi
kujibu madai ya mitandao ya kijamii kuwa alitumia vyeti vya mtu cha
kidato cha nne, Askofu Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ameibuka na
kusema kuwa ni kweli alitumia vyeti hivyo.
Askofu
Gwajima amesema kuwa anamfahamu sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na
kuwa jina lake halisi ni Daudi Bashite na kwamba hilo la Paul Makonda ni
la mwenye vyeti hivyo.
Aidha,
Askofu Gwajima amedai kuwa anavyovyeti vya Daudi Bashite vinavyoonyesha
kuwa hakufaulu na kwamba atashangaa kama Waziri wa Elimu, Prof.
Ndalichako atalifumbia macho jambo hili.
Pia ametishia kuwa, kama mamlaka husika hazitachukua hatua haraka basi yeye atatoka hadharani na vyeti hivyo.
NA MVUNGI K.A
0 comments:
Post a Comment