Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewaonya walioficha Sukari na kutishia
Kuichukua Sukari hiyo na Kuigawa Bure Kwa Wananchi. Rais Magufuli ametoa
onyo kali kwa wafanyabiashara walioficha sukari ili baadae waiuze kwa
bei ya juu.
Amesema wafanyabiashara hao wenye tamaa ya pesa walikuwa wakifuata
sukari iliyo Expire huko Brazili na kuileta nchini ili watengeneze faida
na ndo maana serikali iliwapiga marufuku kuagiza.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akiwasalimia wananchi wa Katesh,
Mkoani Manyara. Rais ametoka Mkoani Dodoma leo, anaelekea Mkoani Arusha
kwa usafiri wa gari.
Akiongea na mamia ya wananchi hao waliojitokeza kumlaki njiani, Rais
Magufuli amewatoa hofu wananchi kuhusu uhaba wa sukari kwa kuwa tayari
wako katika mchakato wa kuagiza makontena ya sukari nje ya nchi ili
kuwakabili wafanyabiashara walioficha bidhaa hiyo.
Amesema kwa taarifa alizonazo, kuna mfanyabiashara alienda akanunua
sukari pale Kilombero zaidi ya tani 3000 na hataki kuzichukua hadi leo
Pia amesema kuna mwingine ana godauni huko Mbagala yenye tani 4000 ambazo hataki kuzitoa ili wananchi wakose sukari.
Rais Magufuli amesema ameviagiza vyombo vya dola viwafuatilie ili
ikithibitika sukari waliificha basi ichukuliwe na kugawiwa bure kwa
wananchi na pia watapigwa marufuku kufanya biashara yoyote hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment