Monday, 25 December 2023

Happy Christmas

👋👼👋 Tunawatakia happy Christmas day wadau wetu wa uhakika nakuwa ahidi juu ya kuwapatieni habari za kina katika kila nyanza, halikadhalika similizi kabambe za kukata na shoka. Mungu awabariki sana 

Share:

Wednesday, 31 May 2017

Mzee Philemon Ndesamburo afariki dunia




Wednesday, May 31, 2017

Breaking News: Mzee Philemon Ndesamburo(CHADEMA) afariki dunia

Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini (Chadema) Philemon Ndesamburo amefariki dunia ghafla leo, wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Moshi.
 
Katibu wa Chadema, Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema amethibitisha kifo hicho na kueleza kuwa wataendelea kutoa taarifa zaidi juu ya kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe.
 
Taarifa zaidi kuhusu kifo cha Ndesamburo zitaendelea kukujia.



Share:

Monday, 1 May 2017

Yaliyojiri Moshi katika maadhimisho siku ya wafanyakazi Duniani


Monday, May 1, 2017

Leo ni maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani, ambapo Tanzania inaunga na nchi nyingine duniani kuadhimisha na Kitaifa maadhimisho hayo yanafanyika katika viwanja vya Ushirika Moshi, mkoani Kilimanjaro na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ndiye mgeni rasmi katika maadhimisho hayo akiwa ameambatana na Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine wa Kitaifa.

Share:

Thursday, 2 March 2017

Askofu Gwajima akataa kuwafungulia polisi mlango

Jeshi  la Polisi kwa mara nyingine jana lilizingira nyumba ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, kwa kile lilichodai kuwa lilifika kufanya uangalizi.

Taarifa ambazo zimethibitishwa na Askofu Gwajima mwenyewe, zinaeleza kuwa polisi walifika nyumbani kwake wakiwa katika gari lao.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, polisi hao walipojaribu kutaka kuingia nyumbani kwa askofu huyo, walizuiwa mlangoni kwa sababu hawakuwa na kibali chochote wala maelezo yanayojitosheleza ya kutaka kukutana na kiongozi huyo wa kiroho.

Askofu Gwajima  jana alikiri polisi hao kumfuata nyumbani kwake na hivyo kulazimika kumtafuta wakili wake mara moja.

“Ni kweli walikuja wakiwa na gari la polisi, lakini walipofika nami nilimpigia mwanasheria wangu ambaye aliniambia tuwaulize wametumwa na nani na kama wana ‘search warrant’ (kibali cha kufanya upekuzi) au ‘arrest warrant’ (kibali cha kukamata),” alisema.

Askofu Gwajima alisema walipowauliza, walimtaja Afande Kingai kama ndiye mtu aliyewatuma, lakini hawakuwa na kibali chochote.

Kwa mujibu wa Askofu Gwajima, mwanasheria wake alifanya mawasiliano ya simu na Afande Kingai ambaye amepewa jukumu la kuwafuatilia wale wote waliotuhumiwa katika sakata la dawa za kulevya na kumuuliza sababu za kumfuata nyumbani.

“Afande Kingai amemweleza mwanasheria wangu kuwa walikuwa wamekuja kwa ajili ya ‘observation’ (uangalizi) tu, kwa hiyo mwanasheria wangu akasema kama ni ‘observation’ tu tusiwaruhusu kuingia ndani kwa sababu sheria ya hivyo hakuna, na sisi tumewazuia hawakuingia ndani,” alisema Askofu Gwajima.

Alipoulizwa kama kufuatwa kwake sasa na polisi kuna uhusiano wowote na kauli alizozitoa kanisani kwake hivi karibuni kuhusu elimu ya Paul Makonda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Askofu Gwajima alisema huenda ikawa hivyo, lakini akasisitiza kuwa hana uhakika kwa sababu hajazungumza na askari waliomfuata.

Na alipoulizwa kama anadhani ujio huo pia unatokana na andiko ambalo linasambaa kwenye mitandao ya kijamii ambalo linasema Jumapili ijayo mwalimu aliyemfundisha mtu mmoja anayetajwa kwa jina la Bashite atakuwapo kanisani kutoa ushuhuda, Askofu Gwajima alikana akisema andiko hilo si lake.

Pamoja na hayo, Askofu Gwajima alikwenda mbali na kuhoji: “Hata kama ni kweli, sasa unaogopa mwalimu kuja… kanisani kwangu wapo watu wengi waliosoma naye Bashite kuanzia shule ya msingi na Sekondari ya Pamba… vyeti kama huna huna tu.”

Alipoulizwa haoni kauli yake kwamba Rais Magufuli ni tofauti kabisa na Makonda ilikuwa na nia ya kuwatenganisha viongozi hao, Askofu Gwajima alisema aliyemtaja kwa kumshambulia ni Makonda na si Rais.

“Aliyenitaja kwa kunishambulia katika sakata la dawa za kulevya ni Makonda na si Rais, mimi nimemuongelea Makonda, mimi ni mtumishi wa Mungu siwezi kuongozwa kwa ‘speculation’, si unajua hata Yesu alisema kama wewe huna dhambi basi uwe wa kwanza kushika jiwe,” alisema Askofu Gwajima.

Alipoelezwa kuwa katika mahubiri yake ni kama anaonekana kumshtaki Makonda, askofu huyo alisema: “Nilisema nitamshtaki kwa mahakama iliyo juu yake na nilisema Makonda aombe radhi, angekuwa mstaarabu baada ya sakata lile yeye mwenyewe angenipigia simu na kuniambia Gwajima nilikengeuka, lakini hajafanya hivyo.”
 
Pamoja na hayo, Askofu Gwajima alisema kwa aliyoyafanya Makonda tayari amekwishamsamehe na ndiyo maana hajampeleka mahakamani.

Share:

Monday, 27 February 2017

ASKOFU GWAJIMA AONYESHA VYETI FEKI VYA MAKONDA

Siku kadhaa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kusema kuwa hawezi kujibu madai ya mitandao ya kijamii kuwa alitumia vyeti vya mtu cha kidato cha nne, Askofu Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ameibuka na kusema kuwa ni kweli alitumia vyeti hivyo.

Askofu Gwajima amesema kuwa anamfahamu sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuwa jina lake halisi ni Daudi Bashite na kwamba hilo la Paul Makonda ni la mwenye vyeti hivyo.

Aidha, Askofu Gwajima amedai kuwa anavyovyeti vya Daudi Bashite vinavyoonyesha kuwa hakufaulu na kwamba atashangaa kama Waziri wa Elimu, Prof. Ndalichako atalifumbia macho jambo hili. 
Pia ametishia kuwa, kama mamlaka husika hazitachukua hatua haraka basi yeye atatoka hadharani na vyeti hivyo.
 
NA MVUNGI K.A

Share:

Sunday, 26 February 2017

MAKONDA AOMBEWA NA WAUMINI WA DINI ZOTE



Paul Makonda Adai Kuna Watu 12 Walikuwa Wamepanga Njama za Kumtupia Majini...


Mkuu wa mkoa wa Dar, Paul Makonda amesema katika vita ya watu wanaojihusisha na dawa za kulevya, kuna waumini 12 walikuwa wamepanga njama za kutaka kumtupia majini lakini hawajafanikiwa kutokana na maombi ya viongozi wa dini.

Amedai waumini hao waliandaa mbuzi mweupe ili kumtoa kafara na aliwatambua kupitia mtandao wake.

Makonda amesema haamini kama waliofanya hivyo walikuwa ni Waislamu, bali kundi la watu waliokuwa wamevaa kanzu kwa utambulisho huo na kwamba huenda walitumika kuwalia watu fedha zao.
by Mvungi K. A
Share:

MBUNGE WA BABATI- MH. PAULINA GEKULI ANUSURIKA KIFO

Sunday, February 26, 2017

Mbunge Paulina Gekul anusurika Kifo......Alazwa ICU, Ziara yaahirishwa

Mbunge wa jimbo la Babati mjini Paulina Gekul nusra kupoteza maisha yake baada ya gari lake lenye namba za usajili T 189 BHQ kupata ajali.
Inasemekana chanzo cha ajali hiyo ni gari kuacha njia na kupinduka vibaya ambapo mbunge huyo alikuwa katika msafara wa naibu waziri wa Mazingira Luhaga Mpina wilayani Babati mkoa wa Manyara.

Baada ya ajali hii kutokea mmbunge Paulina Gekul ambaye ni mmbunge wa babati mjini akakimbizwa hospitali ya mkoa wa manyara na kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi I.C.U huku wanahabari wakikatazwa kuingia katika chumba hiki na madakatari ambao wanamuhudumia mbunge huyo 
 
Hata hivyo baada ya ajali kutokea naibu waziri wa mazingira amelazimika kuahirisha ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya mji wa babati huku mpina akiipongeza halmasahauri ya mji wa babati kwa kutambua umuhimu wa kutunza mazingira katika hali ya usafi baada ya kununua gari kwaajili ya kubebea taka lenye thamani ya zaidi ya milioni 200.

NA MVUNGI K.A
Share:

Tuesday, 21 February 2017

FID Q HAWEZI FREESTYLE – Young Killer


YOUNG KILLER AMTOLEA POVU NGOSHA

Rapa Young Killer Msodoki amefunguka na kusema hajawahi kumkubali rapa Fareed Kubanda  Fid Q kwenye kufanya mitindo huru kwa kuwa hajawahi kumuona mkali huyo wa hip hop Bongo akifanya mitindo huru.
Young Killer alisema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema yeye anawakubali sana Nikki Mbishi, Godzilah pamoja na marehemu Albert Mangwea kwa kufanya ‘Free style’ sababu anatambua uwezo wao katika nyanja hiyo.
“Sijawahi kumkubali Fid Q kwa ‘free style’ sababu sijawahi kumuona akifanya hivyo ila niliowahi kuwaona wakifanya mitindo huru nampenda sana Nikki Mbishi, GodZillah pamoja marehemu Albert Magwea” alisema Young Killer
Mba na hilo Young Killer amesema baada ya kufanya kazi na Fid Q msanii mwingine wa hip hop anayetamani kufanya naye kazi kwa sasa ni Mbunge wa mikumi ‘Prof Jay’.
“Kiukweli kabisa kwa sasa hivi mimi natamani sana kufanya kazi na Prof Jay, hata hivyo tayari nipo kwenye mipango ya kufanya kazi na rapper Chemical “. Aliongeza  Young Killer.
eatv.tv

Share:

Nay wamitego atangaza nia ya kuanzisha kanisa.


Tuesday, February 21, 2017

Msani wa bongo fleva Nay wa mitego atangaza nia yake ya kuanzisha kanisa takatifu. 
 
Anadai kua kanisa lake halitakua la upigaji wa mkwanja kama makanisa feki yanavyofanya.
 
“Acha kanisa likamilike, mwenye Mungu asimamie tutajua nini kinaenda kutokea lakini sio kanisa kwaajili ya kupiga hela,” Nay aliiambia E-News.
 
Nay amedai kuwa mchungaji wa kanisa lake atakuwa tofauti na hatotegemea sadaka za waumini ili kuendesha maisha yake, bali kazi yake nyingine itakayoweza kumuingizia kipato.
Rapper huyo amejinadi kuwa anatarajia kupata waumini wengi kupitia kanisa lake na kwamba litakuwa chanzo cha mafanikio katika mambo yao.
 
Nay amedai kuwa kanisa lake litajengwa Mbezi ya Kimara jijini Dar es Salaam.

Share:

Tuesday, 24 January 2017

TANZANIA KYATANGAZA KUTOPOKEA WAKIMBIZI

Serikali imetangaza kusimamisha kupokea wakimbizi kutoka nchi za Maziwa Makuu kwa makundi, kutokana na kutokuwepo kwa sababu za kiusalama, zinazowafanya wakimbizi hao kukimbia nchi zao na kuomba hifadhi ya ukimbizi nchini.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ametoa kauli hiyo ya serikali mjini Kigoma wakati wa uteketezaji wa silaha haramu, lililofanyika kikanda mkoani Kigoma, na kueleza kuwa kwa sasa hakuna tena wakimbizi watakaoingia kwa makundi watakaoruhusiwa kuingia nchini.

Mwigulu alisema serikali itawapokea wakimbizi mmoja mmoja na kila atakayeingia atahojiwa na mamlaka zinazohusika na mamlaka zikijiridhisha kuwa anastahili hadhi ya ukimbizi, atapokewa na kupelekwa kwenye kambi za wakimbizi zilizopo, kwani hakuna tena kambi ya wakimbizi itakayofunguliwa kwa sasa.

Alisema serikali kwa kutumia vyombo vyake, imejiridhisha kwamba hakuna hali mbaya ya usalama, inayowakimbiza raia hao kutoka kwenye nchi zao na kwamba zaidi imegundulika kuwa wengi wao wanakimbia kwa sababu za kiuchumi, kuja kutafuta namna ya kuishi ili kukidhi hali zao za maisha.

Alisema uwepo na uingiaji wa wakimbizi nchini, umekuwa na mchango mkubwa katika uzagaaji wa silaha haramu sanjari na kuongezeka kwa matukio ya utumiaji wa silaha na kuathiri uchumi na maisha ya watu mbalimbali.

Katika hatua nyingine, waziri huyo amesema serikali imefuta utaratibu wa kutoa uraia kwa makundi, kama ilivyofanya kwa wakimbizi wa Burundi waliopo nchini. Alisema kwamba kwa sasa uraia utatolewa kwa mtu kulingana na maombi yake.

Alisema ukarimu huo wa Watanzania, umekuwa na athari kubwa katika ulinzi na usalama nchini, hasa mikoa ambayo imewahifadhi watu hao kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya mauaji, ujambazi wa kutumia bunduki, lakini kupanda mbegu mbaya ya kuuana kwa kulipiza visasi ambavyo vimekuwa vikifanywa na raia hao waliopewa uraia.

“Kwa mamlaka niliyopewa, natoa amri ya kusimamisha kutoa uraia kwa makundi kama ambavyo imetoa Tanzania na haijawahi kutokea nchi nyingine, tumeona athari kubwa ya watu hao na sasa sehemu kubwa ya Mkoa wa Tabora imekuwa na hali mbaya kiusalama na tabia ya kulipizana visasi,” alieleza Mwigulu.

Akitoa taarifa kwa waziri, Kamishna wa Mafunzo na Operesheni wa Jeshi la Polisi, Marijani Nsato alisema silaha haramu 5,608 zikiwemo bunduki za kivita, zilitarajia kuteketezwa. Nsato alisema katika silaha hizo, kulikuwa na bastola 21, Shortgun 606, SMG 166, Riffle 300, bastola bandia 21, FN Riffle 3, G3 moja, SAR 3 na magobore 4487.

Sanjali na bunduki hizo, aliitaja mikoa ambayo imeshiriki katika kuchangia bunduki haramu zilizoteketezwa kuwa ni Kagera 100, Rukwa 189, Katavi 81, Simiyu 16, Mwanza 88, Geita 82, Mara 80 na Kigoma ukiwa na jumla ya bunduki 424 ambazo zimeteketezwa katika kazi ya jana.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Emmanuel Maganga alisema mkoa huo kuwa mpakani na kupokea idadi kubwa ya wakimbizi kutoka nchi za Maziwa Makuu, kumechangia mkoa huo kuathirika kwa kiasi kikubwa na uzagaaji silaha haramu na matukio ya ujambazi kwa kutumia silaha.

Alisema mkoa utaendelea kuweka mkakati wa kudhibiti silaha haramu na matukio ya ujambazi wa kutumia silaha.

Share:

Total Pageviews

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

CEO:KOMBO MVUNGI




HOTLINE:+255719050552 +255762198234


Email:mvungi134family@gmail.com

Dodoma,Tanzania

KARIBU UTANGAZE BIASHARA YAKO BEI NI NAFUU
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Blog Archive

My Blog List

Powered by Blogger.